WASIFU WA BALOZI ISAAC ABRAHAM SEPETU
Balozi Isaac Abraham Sepetu alizaliwa Oktoba 16, 1943 mkoani Tabora na kabila lake ni Myamwezi.
Alihamia Visiwani Zanzibar alipokulia na kupata elimu yake chini ya
uangalizi wa Said Sepetu Langa pamoja na Mzee Abeid Amaan Karume
aliyekuwa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
1952 - 1963 Balozi Sepetu alipata elimu ya msingi katika Shule ya Mt. Joseph iliyopo Zanzibar.
1964-1970 Alijiunga na Chuo Kikuu cha Berlin, Ujerumani na kupata
Shahada ya Uzamili katika Uchumi (Masters Degree in Economics).
1971-1972 Balozi Sepetu aliajiriwa katika Serekali ya Mapinduzi
Zanzibar akiwa Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi wa Shirika la Biashara ya
Nje Zanzibar.
Pia aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ikulu ya Zanzibar.
1972-1977 Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1977-1979 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Habri na Utangazaji katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1979-1982 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1982- 1989 Aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania katika Shirikisho la Usoviet (Soviet Union).
1989-1990 Aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zaire.
1990-2000 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Mipango katika Serekali ya Mapinduzi Zanzibar.
Pia aliwahi kuwa Mshauri wa Rais katika Ushirikiano wa Kimataifa
kwenye Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu wa Tume ya pamoja ya
(IPC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
Balozi Sepetu aliwahi pia kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.
0 comments:
Post a Comment