Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Saturday, December 8, 2012

TOP TEN YA WALIOJAALIWA 'MIZIGO'

 

Anautajiri wa dola milioni $250 ,jinsi gani alipata hu utajiri,?? Nikutokana na uigizaji wake, Mfanyabiashara na kazi yake ya uimbaji. J-lo ni mwanada maaraufu mwenye maumbile makubwa ya makalio, ambayo yanafanya ashikile nafasi ya kwanza kwenye orodha ya wanawake maarufu Hollywood. Inarepotiwa kuwa mataka yake ameya weka bima ya dola milioni $27. Anapenda kujivunia kuonyesha assets yake hiyo kwenye magazines cover ya Stuff magazine mwaka 2001. Ambalo ni moja ya magazine iliyoweka histori ya rekodi ya gazeti lilouza kuliko. Kiukweli hilo tako limegharimu maelfu ya dola na sio chini ya hapo. Matako mengine ya nakuja na kuondoka lakini kwa Jlo atatumia kila kitu kulinda tako lake. Lol

No.2 Kim Kardashian
Anautajiri wa dola milioni $35, jinsi alivyo upata huo utajiri, ?? utajiriwake umetokana , umodel, uigizaji, mwanamkemfanyabiashara, Television Personality, na socialite. Anachukuwa nafasi ya pili kuwa ni mwanamke mwenye Tako kubwa Hollywood, nalilionekana sana kwenye s*x tape ambayo alikuwa nimmoja ya maboyfriend wake maarafu sana. Naalishazushiwa kuwa matako yake ni yakutengeza lakini yeye alikataa akasema no way its real.

3. Beyonce.
Anamiliki utajiri wa dola milioni $300 milioni. Jinsi gani alivyotengeneza utajiri?? Dada huyu anaingiza pesa zake kwa kuwa muandishi mzuri wa nyimbo, rekodi Producer, muigizaji, umodel, mvumbuzi wa mavazi, na ni mfanyabiashara. Anajiita “b**t-y-l-i-c-i-o-u-s” . Nahuyu anachukua nafasi ya 3 kwa kuwa na matako makubwa Hollywood

No.4 Serena Williams
Anautajiri wa dola miliobi $85, nautajiri wake unatokana na uchezaji wa Tennis as Professional. Na nimaarufu kwa kwa kuwa na tako kubwa kwenye tennis, lakini kutoka kwa serena mwnyewe anasema kuna mwanamke mwenye matako makubwa kuliko yangu huko nje nikisimama nae ni aibu tu.

No.5 Nicki Minaj
Anautajiri wa dola milioni $14 ambao umetokana na uandishi wa mistari yake na rapa, mwanadada huyo anapenda sana kuongelea kuhusu tako kila wakati, hata kwenye interview iliotokea New York post Nicki Minaj alikuwa anaongela kuhusu ruma za utengezaji wa matako yake. “absolutely not” said Nicki Minaj alipokuwa anaulizwa kuhusu matako ya kutengeneza , “people will pick anything to talk about , and that happens to be the thing at the moment’’. Alisema Nicki Minaj.
 
No.6 Vida Guerra
Anautajiri wa dola milioni 2.5 na amazitengeza kupitia kazi yake ya umodel. Wakati hajulikani kama wanawake wengine waliopo kwenye orodha yetu, Nyuma kwa Vida kunamilikiwa na dunia, alishinda FHM’s Best B*tt , kwenye the world award na sio mara moja. Ni model, muimbaji na mwigizaji lakini anajivunia kwa kujilikana kwa umbo la mwili wake. Kiukweli ameshinda tuzo ya best b*tt mara mbili .
 
No.7 Nicole “Coco” Austin
Anautajiri wa dola milioni 4 kutokana na umodel, reality Tv Personality , web personality. Hakuna wasi wasi wowote kuwa Mke wa Ice T , Nicole Coco Austine anajivunia mwili wake sana. Anapenda kupost picha za makalio yake sana kwenye Twitter,

No.8 Buffie Carruth
Buffie Carruth vile vile anajulikana kwa jina la Buffie The Body or simply Buffie, ni model kutokea Athens, Georgia anajulikana kunekana kwenye posing za hip hop zinaendana na magazine na kuonekana kwenye video za hip hop. Shukuru kwa model kama Buffie The Body the Big Booty” comple imefagia Us nzima nao inelekea to getting out of control.
 
No.9 Jessica Biel
Anautajiri wa dola milioni $ 18 , amepatamafanikio hayo kwa kuwa muigizaji, model na mwimbaji , anachukua nafasi ya 9 kwa kuwa na makalio makubwa kwa wanawake maarufu. Alianza kucheza kwenye tv kama mtoto wakike wa muhubiri. Lakini umaarufu wake ulitoke bada yakupiga picha ya utupu kwenye Gear Magazine akiwa na umri wa miaka 17.
 
10. Sofia Vergara
Anamiliki utajiri wa dola milioni 14, na utajiri huo unatokana na uigizaji, modeling , mtangazaji wa television na mjasiriamali. Ni muigiza wa modern family amefungasha kila mahali. Ni mdada mwenye kipaji, mzuri na ana makalio mazuri yenye mvuto sana. Ame shikilia namba tatu kwenye Askmen.com 99 Most Desirable Women wa 2011

11.Melyssa Ford
Anamiliki wa dola milioni 2. Na utajiri huo umetokana na uigizaji na umodeling , anashikilia nafasi ya 11 kwa kubarikiwa na tako nzuri. Kiukweli anajulikana kuwa naumbo zuri lenye mbinuko. Ameonyesha anavyotingisha matako yake kwenye vido ya Jay-Z, Ghostface killah, na Mystikal, anajulikana mwanamke mweusi mzuri sana duniani.

No.12 Eva Mendes
Anamiliki utajiri wa dola milioni 12. Ambazo amazitengeza kwa kazi zake za uigizaji, model, uimbaji na ububifu. Eva Mendes maumbile yake yanaweza kumbadilishi shoga kuwa mwanaume waukeli, eva aliamuwa kutikisa dunia baada ya kutoka kwenye Peta akiwa mtupu. Kampeni ilifanyika rockeffeller Plaza. Like mamlaka ya jiji ili waambia waandaji wasi to mda kamili au sehemu itakapofanyika maana walikuwa wanaogopa kutengeneza Mob scene.

No.13 Halle Berry
Anamiliki utajiri wa dola milioni $70 , ambazo zinatokana na uigizaji , na ni former model anachukua nafasi ya 13 kwa kuwa na makalio makubwa holly wood. Na kucheza kwake kwenye movie ya swordfish na monster’s ball imemfanya halle Berry’s kutikisa Hollywood na kwenye orodha yetu anatinngisha pia kwa kuwa na makalio makubwa ndani ya Hollywood.
 
No.14 Scarlett Johansson.
Anautajiri wa dola milioni 35 ambazo amazitengeza kutokana na uigizaji wa movie. Anachukua nafasi ya 14 ya wanawake wenye makalio makubwa Hollywood, anamwili wenye mvuto sana kwenye big scree, ana anajivunia kuwa nao, na haya ni maneno yake. “im curvy-I’m never going to be 5’11 and 120 pounds” “ but I feel lucky to have what I have got” na tunafurahia kumuangalia lol

15. Shakira
Anautajiri wa dola milioni 140 ambazo amaezitengeza kwa kuwa mwimbaji, na mtunzi mzuri wa nyimbo na record producer. Hakukosea kusema Hips don’t lie na hata makalio yake vile never lie. Alichukua nafasi ya tatu kwenye Vote poll ya dunia ya best butt. Ya mtandao wa WENN.com. shakira alifunika kwenye album Laundry Service na kutingisha makalio yake juu ya stage. 
 
Imeandika kwenye http://infosourcestz.wordpress.com

Tuesday, December 4, 2012

ANGALIA PICHA NA MATUKIO YA FINALI ZA MAISHA PLUS BAGAMOYO.

wakifurahi kwa pamojaPlatnum na Masudi Kipanya...

Diamond akiongea mawili,matatu kwa washiriki wa Maisha Plus pamoja na watu wote waliyoudhulia
Platnum akipokea zawadi kutoka kwa Babu wa Kijiji cha Maisha Plus....
  Top 5 ya Maisha Plus
Top 5 wakiwa kizimbani...
Baadhi ya viongozi waliyoudhulia Final hizo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo
Huyu ndiye Mshindi wa Maisha Plus akiwa na Babu baada ya kutangazwa kuwa mshindi

Washiriki,Watu mbalimbali wakimpongeza Mshindi wa Maisha Plus....

EWURA YAFUNGUKA YATANGAZA BEI YA MAFUTA TENA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA
JUMATANO, TAREHE 5 DISEMBA 2012
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 5 Disemba 2012. Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo.
(a) Bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 07 Novemba 2012. 
Katika toleo hili, bei za rejareja kwa Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa viwango vifuatavyo: Petroli Sh 70/lita sawa na asilimia 3.4; Dizeli Sh 10/lita sawa na asilimia 0.53. 
Bei ya Mafuta ya Taa imepungua kwa Sh 3/lita sawa na asilimia 0.1. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimeongezeka kama ifuatavyo: Petroli kwa Sh 69.56/lita sawa na asilimia 3.52; Dizeli kwa Sh 10.04/lita sawa na asilimia 0.52. 
Bei ya Mafuta ya Taa imepungua kwa Sh 3/lita sawa na asilimia 0.15. Mabadiliko haya ya bei yametokana na ongezeko la bei ya mafuta katika soko la dunia na kushuka kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.
(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.
(c) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la tarehe 23 Desemba 2011.
(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.
 Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.
(e) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

Saturday, December 1, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI YALIYOFANYIKA KITAIFA MKOANI LINDI LEO

Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu Mjini Lindi, huku wadau mbalimbali wa masuala ya mapambano ya ukimwi wakishiriki kwa kufanya maonyesho na kutoa elimu na maelezo mbalimbali yanayohusu mapambano ya ukimwi, Rais Pia ameshuhudia utiwaji saini wa msaada wa Dola za Kimarekani Milioni 308 kutoka mfuko wa Global Fund uliosainiwa kati ya Katibu katibu wa Ofisi ya rais Paniel Lyimo na Ramadhan Kijahkati Kabu Mkuu Wizara ya Fedha huku Mfuko wa Global Fund ukiwakilishwa na Christoph Benn Mkurugenzi wa mfuko huo. 
Christoph Benn Mkurugenzi wa mfuko Global Fund akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya wananchi wa mkoa wa Lindi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani iliyofanyika mjini Lindi leo . kutoka kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi TACAIDS Fatuma Mrisho na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila
Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya wananchi wa mkoa wa Lindi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani iliyofanyika mjini Lindi leo . kutoka kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Hussein Mwinyi, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi TACAIDS,Fatuma Mrisho. 
Rais Jakaya Kikwete akishuhudia Utiwaji wa Saini wa msaada wa dola za Kimarekani milioni 308 kwa ajili ya mapambano ya Ukimwi nchini, mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Paniel Lyimo kushoto na Ramadhan Kijah katikati, kulia ni Christoph Benn mkurugenzi wa Mfuko wa Global Fund, waliosimama nyuma kushoto ni Mkewa Rasi Mama Salma Kikwete, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na kulia ni Ursula Muller Mjumbe wa bodi ya The Global Fund,
Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiingia kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi tayari kwa kushiriki katika maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani ambayo yamefanyika mkoani Lindi kitaifa.kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TACAIDS Fatma Mrisho na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila
Rais Jakaya Kikwete akimuonyesha jambo Mkurugenzi wa tume ya kudhibiti Ukimwi Fatma Mrisho wakati alipotembelea mabanda mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani mjini Lindi leo.
Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Bw.Rajab Mwenda afisa masoko wa Mpango wa damu Salama wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani mjini Lindi leo.
Baadhi ya viongozi wa Dini na waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho hayo wakifuatilia kwa karibu matukio yaliyokuwa yakiendelea katika maadhimisho hayo.
Waheshimiwa viongozi wa serikali na baadhi ya wabunge wakiwa katika maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mwakilishi wa mfuko wa bima ya Afya ya Jamii mjini Lindi NHIF Bi. Fortunata Raymond wa tatu kutoka kulia akiongoza maandamano ya wafanyakazi wa mfuko huo katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani.
Kikundi cha matarumbeta kikiongoza maandamano hayo yaliyokuwa yakipita mbele ya Rais kwenye uwanja wa Ilulu leo mjini Lindi.
Kikundi cha kuigiza kutoka mfuko wa bima ya afya ya Jamiii NHIF kikiwapa ujumbe wananchi wqa mkoa wa Lindikuhusu maambukizi ya ukimwi
Kikundi cha ngoza za asili kutoka mkoani Lindi kkitumuiza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi
Mhashamu Baba Askofu Bruno Ngonyani wa Jimbo Katoliki Lindi akifanya maombi rasmi kwa ajili ya kuwakumbuka waliokufa kwa ugonjwa wa ukimwi na kuliombea taifa na wananchi wake kuepuka ugonjwa wa ukimwi na mapambano dhidi ya Ukimwi.PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM

Friday, November 30, 2012

WASANII WA BONGO FLAVA NA HIP HOP, WALALAMIKIWA KUTOHUDHURIA MAZISHI YA SHARO MILIONEA. December 1, 2012



Kupitia  kituo cha luninga cha EATV ndani ya kipindi cha Frieday Night Live jana, kuna malalamishi kibao yaliyojitokeza kwa baadhi ya wasanii wa kike waliokuwa wakihojiwa katika kipindi hicho.

Wasanii hao wakike wawili walionekana kukelwa na kushangazwa na kitendo cha wasanii wa miondoko ya bongo Flava hapa nchini kutojitokeza kabisaa katika mazishi ya msanii mwenzao
Hussein Sharo milionea aliyepata ajali tarehe 26 majira ya saa mblili za usiku mkoani Tanga na kupoteza maisha hapo hapo.

Wadada hao walili wakionekana
EAST AFRICA TV wakiongea kwa kuchungu, walidai kuwa wasanii wa hip hop nao waliohudhuria msiba wa Sharo Milionea walikuwa  wa kuhesabu kama Mwana FA, Roma, Ney wa Mitego Shetta na wengine.

Walidai kuhuzunishwa sana kwani wasanii wakubwa ambao pia walitajwa kutohudhuria msiba huo ni pamoja na
AY, Lady Jay Dee, Bob Junior, Timbulo, PNC, Dogo Janja, DJ Choka, Weusi na wasanii kibao. Mtangazaji wa kipindi hicho pia Sam Misago alishangazwa na kitendo cha wasanii wa hip hop kuto hata zungumzia msiba wa msanii Sharo milionea bali walionekana kufanya yao na kutoona umuhimu wa kuhudhulia msiba huo.

Wadada hao walidai kuwa kila msanii wa Bongo anamfahamu meneja wa Sharo Milionea maarufu kwa jina la
HK, meneja ambaye amekuwa akifanya kazi na wasanii kibao.Ni kwanini wakati amefikwa na msiba wa Sharo Milionea hakuna hata msanii mmoja aliyempigia simu kumpatia pole! hata kama walishindwa kuhudhulia msiba huo?

Katika upande wa
Comedy walidai wasanii wote hawakuhudhulia msiba wa Sharo milionea, kitu ambacho kimewakera sana na kuwaasa kujitokeza katika matatizo ya yanapokuwa yamejitokeza kwani na wao wakipata matatizo hayo watahudhuriwa na nani?

Yapo mengi zaidi yaliyozungumziwa katika kipindi hicho cha
Frieday Night Live ya East Africa TV

MASHUJAA BAND WAPATA AIBU YA KARNE

Kiiipe Yayooo...! Mwanamuziki JB Mpiana na bendi yake wakifanya vitu vyao baada ya kupanda stejini kwenye viwanja vya Leaders Club, Kionondoni jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Hapa ilikuwa ni mida ya saa 9:00 baada ya gwiji huyu kusubiri sana kutokana na mizinguo ya umeme wa TANESCO na pia wa jenereta kubwa lililotegemewa mahala hapo kuzalishia nishati hiyo usiku wa kuamkia leo (Desemba 1, 2012).

Litapona kweli...? Watu wakiwa wamelizunguka jenereta lililokuwa linawazingua wakati wa uzinduzi uliofeli wa albamu ya pili ya mashujaa kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumamosi (Desemba 1, 2012). (Picha: Zote kwa Hisani ya issamichuzi.com)
Gundu la aina yake limeikumba bendi ya Mashujaa inayoundwa na wanamuziki kadhaanyota akiwamo Chaz Baba baada ya uzinduzi wake kukwama usiku wa kuamkia leo kutokana na kukatika hovyo kwa umeme wa TANESCO na pia 'mizinguo' ya kuwaka na kuzima kila mara kwa jenereta kubwa liliotarajiwa kutoa huduma ya nishati hiyo kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa mizinguo hiyo ya umeme ilimchanganya kuliko kawaida mmiliki wa bendi ya Mashujaa, Mamaa Sakina, ambaye inasemekana alianguka na kupoteza fahamu kiasi cha kukimbiziwa hospitali akiwa hoi.

Tatizo hilo lilidumu kwa masaa kibao na kuwafanya mafundi kuihangaikia jenereta huku na huko huku mwanamuziki wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyealikwa kusindikiza uzinduzi wa albamu hiyo, JB Mpiana akilazimika kusubiri sana -- hadi mishale ya saa 9:00 usiku -- ndipo alipopata nafasi ya kupanda jukwaani na kundi lake kufanya kazi iliyowapa fursa ya kutua nchini kwa mbwembwe.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki walishakereka mida hiyo na kutimkia zao, hivyo kukosa uhondo uliotarajiwa katika onyesho hilo ambalo awali lilikuwa na ratiba 'tamu' sana kwa wapenzi wa burudani.

Hakukuwa na taarifa za kina kuhusiana na hali ya kiafya ya Mamaa Sakina hadi kufikia leo asubuhi ya leo (Jumamosi Desemba 1, 2012); kwa mujibu wa EMMANUEL SHILATU

TANZANIA YAITAKA CNN KUACHA UPOTOSHAJI JUU YA MPAKA WA TANZANIA NA MALAWI



    
 
                                            Serikali ya Tanzania imekitaka kituo cha televisheni cha Kimataifa cha CNN kusahihisha taarifa potofu ilizotoa kuhusu mgogoro wa mpaka unaoendelea kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa.

Taarifa hizo zinaonyesha kwamba mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa upo kwenye ufukwe wa Pwani ya Tanzania jambo ambalo Serikali imesema siyo sahihi.

Akiongea na waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Assah Mwambene amesema Serikali ya Tanzania imesikitishwa sana na taarifa hiyo na kuitaka CNN kuisahihisha mara moja.

“Tumesikitishwa sana na taarifa hiyo na tunashangaa kuona chombo kikubwa kama CNN wanaweza kutoa taarifa za uongo kwa kiasi hicho” amesema Bw. Mwambene.

Amesema ukweli ni kwamba unapozungumia eneo la Tanzania kilometa za mraba 947,300 (947,300 sq km)  ikiwa ni pamoja na  nusu ya eneo la ziwa kaskazini mwa mpaka wa Tanzania na Msumbiji na kwamba mpaka upo katikati ya ziwa kama ilivyo kwa mpaka wa Malawi na Msumbiji.
Kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 24 Novemba, 2012, CNN International yenye makao yake Makuu nchini Marekani  imekuwa ikiendesha  kipindi kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi na kuonyesha kwamba mpaka uko pembezoni mwa ufukwe wa Tanzania.

Bw. Mwambene amesema kuwa suala hilo hivi sasa linatarajiwa kupelekwa katika Baraza la Marais wastaafu wa Nchi za Umoja wa SADC kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi.

Wakati huo huo, Sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania bara zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9 mwaka huu.
Kauli mbiu za sherehe za uhuru mwaka huu ni uwajibikaji , uadilifu na uzalendo ni nguzo ya maendeleo ya Taifa letu.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI

Wednesday, November 28, 2012

safari ya mwisho ya mpendwa wetu sharo milionea mchana wa leo

 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele 
 Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.Picha Kwa Hisani ya Jiachie Blog

Thursday, November 22, 2012

Kitabu kipya cha Hadithi| Miss Tanzania.

Katika kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka Masimulizi Entertainment wanakuletea kitabu cha hadithi ya Miss Tanzania amabayo ni tamu na itakusisimua zaidi kuliko ulivyo tarajia. Kitabu hichi cha masimulizi kitatoka na kuingia sokoni hivi karibuni. Kuweka oda yako mapema, wasiliana na MASIMULIZI Blog kupitia 0755 780131, 0764 294499, 0658 780131


Cheki Dude lililodondoka usiku wa manane Kijiji cha Ruganzo wilayani Ngara mkoani Kagera na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi.

 
Kitu kinachosadikiwa ni bomu

     Wataalamu wa mabomu kutoka Jehsi la wananchi wa Tanzania JWTZ kambi ya Biharamulo wameanza kazi ya kukagua kitu ambacho kimeanguka kwenye eneo la Ruganzo wilayani Ngara mkoani  Kagera.

Kituo hicho ambacho baadhi ya watu wanasadiki kuwa ni bomu kina ukubwa wa sentimeta 50 na umbo kama la yai huku kikiwa na nyuzinyuizi kimeanguka jana usiku katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu amesema wataalamu hao wa mbomu ndio watabaini kitu hicho na kuweza kukitolea maelezo pmoja na hatua za kuchukua.
 
Wapo waliodhani kuwa kitu hicho
ni Kombora la masafa marefu
 lililorushwa kutoka nje ya Nchi

 Ni kitu kisichofahamika ni nini, Wapo waliodhani kuwa kitu hicho ni Kombora la masafa marefu lililorushwa kutoka nje ya Nchi,wapo waliodhani kuwa ni Kimondo,wapo wanaodhani kuwa ni Satelite!..LAKINI  Majibu yatatolewa katika Ripoti itakayotolewa na timu/kikosi cha wanajeshi naohusika na masuala ya Mlipuko. tayari kikosi kutoka Biharamulo kimeagizwa KUCHUNGUZA.

Eneo la Ruganzo

   
Kitu hicho kilichondoka kutoka angani hadi ardhini Usiku wa Jumatano November 21 kuamkia Alhamisi November 22, 2012 saa nane Usiku na  kuleta kishindo kikubwa kilichopelekea hali inayofanana na tetemeko la ardhi,wakazi wengi wa eneo la Ruganzo kata ya Kibimba wilayani  Ngara mkoani Kagera  wamekumbwa na hofu kutokana na kitu hicho.
Aidha  kwa mujibu wa mkuu wa Ngara Bw.Kanyasu AMEPIGIWA SIMU NA MAAFISA WA BURUNDI WAKIMUULIZA JUU YA MIUNGURUMO ILIYOSIKIKA UPANDE WA TANZANIA.

JWTZ WAMESHAFIKA ENEO LA TUKIO NA WANAENDELEA NA UCHUNGUZI ZAIDI. BADO HALIJARIPUKA. HUENDA WAKALITEGUA.
Chanzo:Radio Kwizera FM