Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Wednesday, April 3, 2013

HII NI HATARII:::KANGA MOJA TAZAMA WALIVYOFANYA LAANA KATIKA SHOW YA MSANII DIAMOND HUKO BUKOBA.



Mambo yanayofanywa na hawa wakina dada wanaojiita kanga moja kusema ukweli yanatutia aibu sana japo nao wapo katika kutafuta maisha ila kwa hali hii kusema kweli taifa tunalizika zima zima bila kuliuwa.
Mimi binafsi nimeshahudhuria shoo nyingi za hawa akina dada kwa lengo la kusaka habari huko nimeona mengi ambao mengine si rahisi kuyaanika hapa kutokana na maadili yetu lakini kifupi kinadada hawa wanachofanya mungu atunusuru
Kina dada hawa ambao uchezaji wao hauna tofauti sana na wale wachezaji wa casino maana huvaa kanga moja huku ndani wakiwa wamevaa bikini mfano wa kamba nyembamba kama uzi kisha huimwagia maji au bia  na ikishalowa kabisa huyaanika maungo yao wazi kabisa huku mwenzie akimuingizia chupa nyuma na kisha kuiachia ikisha ingia na mchezaji hucheza nayo na mara nyingine huikalia kwa staili ya kimahaba kana kwamba kakalia mwanume,  Na mara nyingine katika uchezaji wao watu hujikuta wanaona nyuchi zao ila wao hawajali hulewa na sifa za makelele na kujikuta wakiendelea na shoo.
Utafiti wa mtandao huu umebaini kuwa kina dada hawa licha ya kazi ngumu waifanyayo hulipwa ujira mdogo sana ambao haufiki hata laki moja ila kutokana na ugumu wa maisha wamejikuta wakilazimika kufanya kazi hiyo bila kujali

Akizungumza na mtandao huu juzi baada ya shoo waliyofanya na diamond huko bukoba mmoja wa akina dada hilo ambaye hakupenda kutajwa hapa kutokana na kuogopa ataonekana kuwasaliti wenzie alilonga na blog hii pendwa na kusema,Unajua kaka sisi si kama tunapenda kufanya hii kazi ila ugumu wa maisha ndio umetufikisha hapa maana ukituambia tuache hii kazi inamaana unatuambia tukajipange kinondoni makaburini mwananyamala au buguruni kujiuza kitu ambacho sisi tumeshindwa ndio maana tunajitafutia riziki zetu za halali alisema mwadada huyo mapepe kupindukia,mwandishi wetu alipomuhoji wao wanaifundisha nini jamii kwakucheza vile alisema kuwa wao wapo kazini sasa haamini kama mzazi anaweza kwenda sehemu kama ile na mtoto wakati ameshaambiwa kanga moja watakuwepo au wewe kama hupendi shoo shoo hizi sidhani kama utakuja.
Baada ya maswali kadhaa mtandao huu ulitaka kujua wanalipwa kiasi gani kwa shoo ambapo dada huyo alisema Unadhani hata tunalipwa pesa nyingi sana basi pesa yetu ni kama elfu hamsini kwa kila mtu mmoja kwa shoo ila tukisafiri mikowani ndio tunarudi na pesa alisema mwanadada huyo bila kufafanua wanarudi na pesa kivipi
Hii ndio moja ya kazi za dada zetu siku hizi iliyochukuwa umaarufu sana nchini kwa kuteka watu wengi katika shoo zao na kufanya makundi ya namna hiyo kuibuka kila kukicha kwani ni kama wadau au wawekezaji wa sehemu za starehe wamegundua biashara hiyo inawalipa bila kujali madhara kwa taifa hili maana  uchezaji wao wakuwekeana chupa ni sawa nakudhihirisha kuunga mkona vitendo vya ulawiti au ushoga.
Makundi mengine ya dizaini hiyo ni kama Kitu Tigo,Wela Wela,kundi la msanii wa filamu na muziki Shilole Classic, na lile la Sunura Mush ambaye pia ni msanii wa filamu alimfuata shilole katika muziki huo.



















































 

UWOYA NA NDIKUMANA WARUDIANA...ANGALIA PICHA ZAO MBILI WAKIWA KATIKA POZI LA MAHABA

 

 



KUNA maswali tena? Ndoa ya staa kiwango cha juu Bongo, Irene Uwoya na mumewe Hamad Ndikumana 'Kataut' anayeng'ara katika kabumbu akikipiga pande za Rwanda imerejewa na uhai tena..
 
chanzo: emmanuel shilatu

BAADA YA WEMA SEPETU KUMLIPIA FAINI NA KUMUEPUSHA NA JELA, KAJALA AMEAMUA KUFANYA HILI

.


Siku kadhaa baada ya mwigizaji Wema Sepetu kulipa milioni 13 na kumalizana na faini iliyokua inamkabili mwigizaji Kajala aliyotakiwa kulipa Mahakamani baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi yake, mwigizaji Kajala alieguswa na wema wa Wema, ameamua kochora mgongoni tattoo ya jina la Wema.
Wema Sepetu amesema kwamba Kajala alikwenda nyumbani kwake na kuchora hii tattoo bila kumwambia, Wema alipouliza kuna nini mbona kama kuna kitu kinaendelea, Kajala alimwambia mtu wa Tatoo asimwambie mpaka walipomaliza kuchora ndio wakamwonyesha huku Kajala akimwambia Wema ni shujaa wake kwa alichofanya.

Tuesday, April 2, 2013

Maana ya Freestyle (mitindo huru), ‘Freestyle halisi ni ile ya mashairi yaliyoandikwa’ na freestyle sio nguzo ya Hip Hop!


 

NOTE: Freestyle sio nguzo ya Hip Hop kama wengi wanavyosema, ila freestyle iko ndani ya nguzo ya Hip Hop inayoitwa Emceeing (Uchenguaji), ambapo mchenguaji anaweza akafanya mitindo huru.

Wengi wamekuwa wakizungumza kuwa kama mtu hajui ku-freestyle basi sio MC, nakubaliana nao kabisa kwa sababu hakuna MC ambae hajui kufreestyle na hajawahi kutokea, na hapa bongo pia hayupo. Lakini tunafahamu maana halisi ya mitindo huru ama freestyle? Utakubaliana na mimi baada ya kusoma dondoo hizi hadi mwisho.

Maana ya ‘freestyle halisia’

Katika kitabu kinachoitwa ‘How to Rap: The Art & Science of Hip-Hop’, mwana HipHop mkongwe na mfatiliaji wa maswala ya Hip Hop anaeitwa Big Daddy Kane, anaelezea kiundani kuwa freestyle halisia ni ile ya mashairi yanayoandikwa kwanza kisha yanaimbwa lakini inakuwa free of style kwa sababu MC hachaguliwi mada ya kuimba,anaandika kile anachotaka yeye kukiwakilisha katika jamii.

Na hii ilikuwa ni mitindo huru iliyoshika chati sana miaka ya 80, Kane anasema, “Miaka ya 80 tulipokuwa tukisema tunaandika mitindo huru (freestyle), hiyo ilimaanisha ni mashairi uliyokuwa unaandika ambayo yalikuwa ‘free of style’...kimsingi ilikuwa ni mistari ambayo ulikuwa unajisifia na kujikweza wewe mwenyewe.”
 

Mwanaharakati mwingine wa Hip Hop wa miaka hiyo anaeitwa Myke 9, nae aliongeza kwa kusema, “Miaka ile mitindo huru ilikuwa ni kuchana mistari kuhusu kitu chochote bila kupangiwa, na ilikuwa inaandikwa ama kukaririwa.”
Natika kitabu kingine kinachoitwa ‘There’s A God On The Mic’, Kool  Moe anaelezea maana ya freestyle kama mistari iliyoandikwa ambayo mwandishi hachaguliwi mada ya kuzungumzia.

Mfano mzuri, tukiangalia pia hata katika tuzo za hip hop kama zile zinazotolewa na kituo cha runinga cha BET, BET HIP HOP AWARDS, Cypher freestyle, wasanii wote huimba mashairi ambayo waliyaandika kabla ama waliyakariri na hivyo wakati mwingine wenzao kufuatisha kile wanachoimba. 

Freestyle ya mashairi ya Kutoa kichwani papo kwa papo:

Haina maana kuwa mtindo huru wa kutoa mashairi kichwani sio sahihi, lakini huu ni mtindo ambao umezaliwa kutoka katika mitindo huru ya kuandikwa, na wakongwe katika Muziki wa Hip Hop wanasema mtindo huu ulianza miaka ya 90, na uliitwa ‘off the top of the head’. Na hiki kilikuwa ni kipaji kingine kabisa ambacho wengi walikikimbilia walikuwa hawana uwezo wa kuandika mashairi mazuri, lakini wanaweza kutoa maneno kichwani na kuyapanga vizuri kwa vina, hii baadae ilizaa freestyle battle (mashindano ya kughani kwa kutoa mashairi kichwani papo kwa papo) ambayo ilivuma sana na kuwa burudani nyingine katika vilinge (cypher).

Divine Styler anasema, “Katika shule niliyotokea, kufanya mitindo huru ilikuwa ni kuimba mistari iliyoandikwa ambayo haina concept ya kupangiwa.”

Mitindo huru ya Kutoa Kichwani papo kwa papo ilianza lini?

Kool Moe ambae ni mkongwe na mfuatiliaji wa Hip Hop kwa ukaribu sana anaeleza kuwa mitindo huru ya aina hii ya kutoa mashairi kichwani papo kwa papo (off the top of the head), ilianza katikati  ya miaka ya 80, na kushika kasi zaidi baada ya Eminem kutoaa filamu ya 8’ Mile ambayo iliwahamashisha vijana wengi kujiingiza katika aina hiyo ya mitindo huru.

“Hadi mwaka 1986, mitindo huru yote ilikuwa ni ya kuandika mashairi kwanza ama kukariri, ilikuwa ni jinsi gani ungeweza kuja na mashairi mazuri yaliyoandikwa bila kuwa na mada maalum na bila kuwa na sababu ya msingi zaidi ya kuonesha uwezo wako ama ujuzi wako wa kuandika mashairi.”

Wapo wasanii wa hapa bongo wengi sana ambao ni wazuri sana katika kufanya freestyle za kutoa kichwani kama God Zilla, Nikki Mbishi, Young D, Ngwair na wengine wengi. Lakini wapo wengine ambao hawana kipaji cha kutoa mashairi kichwani papo kwa papo lakini ni wakali sana hasa wakiandika mashairi, hii haina maana kuwa kutokuwa na uwezo wa kutoa mashairi kichwani papo kwa papo ni udhaifu katika Hip Hop.
MUCH RESPECT KWA JOSEFLY

Wema Sepetu afunguka sababu ya kumtolea Kajala mil. 13 ili asiende jela miaka mitano, “Naamini what I did is best.”


Wema sepetu ambae amemake headlines mwanzoni mwa wiki hii na kuwaacha midomo wazi watu wengi baada ya kuingia mfukoni na kutoa sh. Million 13 kumsaidia Kajala asiende jela miaka Mitano, amefunguka sababu ya kuchukua uamuzi huo ambao wengi hawakuutegemea.
Wema ameuambia mtandao wa Bongo5 kuwa hakufikiria mara mbili kuchukua uamuzi huo, na hapo amekubali usemi kuwa kutoa ni moyo.

“Kusema kweli wanasemaga kutoa ni moyo so naamini what I did is best”, alifunguka staa huyo wa Bongo Movie.

“Nimefanya kama kumsaidia rafiki yangu kama namsaidia ndugu yangu na sidhani kama ingekuwa kitu kizuri kumuona mwenzako anaingia kwenye dhamana,kwenye tabu, kwenye mateso wakati nina uwezo wa kumsaidia kwa hiyo I just did what I had to do.”

Wema sepetu ni staa wa bongo movie ambae mara nyingi media zimekuwa zikiandika habari controversial kuhusu yeye, lakini kipindi hiki Wema ameonesha moyo mkubwa na wa kipekee alionao kwa kujitolea pesa taslim sh. Million 13 kumsaidia Kajala msanii wa kuigiza ili asiende jela miaka mitano kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa na mahakama.

Uamuzi huu wa Wema umepongezwa sana na mastaa wa muziki na bongo Movie pamoja na wapenzi wa sanaa Tanzania. Kweli kwa hili anastahili pongezi kubwa sana, she made it.
 

Lady Jay Dee achafukwa na roho na kuanzisha kituo chake cha Radio soon, kitaitwa ‘Kwanza FM’.

Baada ya kuwasha moto wenye joto hasira kupitia mtandao wa kijamii wa twitter akiuelekeza kwa kituo kimoja cha radio ‘radio ya watu’ kwa takribani siku 4 hivi. Sasa Lady Jay Dee, Binti Komando ametangaza rasmi kupitia account yake ya twitter kuwa anaanzisha kituo chake mwenyewe cha radio hivi karibuni.

Tweet yake inasomeka, “Kwanza Fm coming soon. Yangu Mwenyewee”. Hii inamaanisha kuwa mmiliki wa ‘Kwanza Fm’ ni yeye binti komando, Lady Jay Dee ambae kupitia tweet zake za hivi karibuni ameongeza a.k.a ya ‘Anaconda’

Jide alijua kabisa kuwa inawezekana watu wakachukulia kama ni April fool’s day na kuchukulia tweet zake kama ni uongo, na hivyo alitoa tahadhari mapema sana kuwa tweet zake hazina uhusiano na April fool’s day na kila kitu ni ukweli, kwa maana hiyo hata radio yake ‘Kwanza FM’ ni kweli.

“Tatizo ni kuwa hata nikitweet vya ukweli mtachukulia ni April fool’s day, Mi nina Tweet vya ukweli ila nyie mtaamua sasa. Sizugi wala nini.” Alitweet Jide.

Lakini kwa kuwa watu wengi wanajua Jay Dee ametokea mkoa wa Mara walianza kuhisi kuwa labda atakuwa Mkurya kwa anaweza kuwa na asili ya hasira kama wengi wanavyoamini, na hapo Jide aliwafafanulia kwa tweet yake.

“Mimi sio mkurya ila nina joto hasira #JotoHasira”

Tunakutakia mafanikio mema zaidi tuongeze kituo kingine cha radio, na hiki kitakuwa cha kwanza kumilikiwa na msanii/mwanamuziki wa kike Tanzania.

Justin Bieber awakomesha TMZ

Justin Bieber ameamua kulipiza kisasi kwa TMZ jana kwenye siku ya wajinga duniani. Website hiyo imekuwa ikimfuatilia staa huyo kila siku kwa habari mbaya na jana aliamua kuwageuzia kibao.
justin_bieber_leather_pants_bl
Jana Bieber alitweet kwa followers wake wafikikao milioni 37, “As promised taking all fan phone calls TODAY at (888) 847 9869. Talk to u soon!” Of course, namba hiyo sio yake bali ni ya TMZ.
Bieber aliongeza tena kwa kuandika, “Did everyone call me yet?” Kwakuwa namba hiyo ni ya bure kupiga (toll free), TMZ watalazimika kulipia bili yake simu zote.
Ripota wa TMZ Dax Holt alitweet: Best April fools joke goes 2 @JustinBieber. He tweeted out TMZs phone # saying he would be taking fan calls. Well played Bieber, well played.”
Aliongeza: The phones here at TMZ won’t stop ringing!!#BieberAprilFoolsJoke LOL! So funny.

chanzo: bongo5

KIJIJI CHA MISUKULE CHAFUMULIWA

Msukule.


Msukule.
Msukule.

Na Makongoro Oging', Bagamoyo
INATISHA na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo  mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi  wa dini kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini kuteua kijiji hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni kuwalaghai waumini kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na kuchukuliwa kimazingara.
Gazeti hili limebaini kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
Habari kutoka kijijini hapo zinadai kwamba viongozi wa dini wanaofika katika kijiji hicho wamekuwa wakiwalipa watu wanaojitokeza kuwa misukule bandia kati ya shilingi 200,000  hadi 250,000  kwa kila mtu.
Msukule.
Imegundulika kuwa viongozi hao wa dini  hufanya zoezi hilo kwa siri kubwa na kuna  nyumba ya mchungaji mmoja, nje kidogo ya kijiji hicho ambapo misukule hao feki  hupewa mafunzo ya nini cha kufanya kabla ya kusafirishwa kuelekea Dar es Saalam.


Imeelezwa kuwa misukule husafirishwa kwenye magari yenye vioo vyeusi ‘tinted’ wakiwa wamepakwa matope mwili mzima  na kuvalishwa nguo zilizochanika.


“Wapo wachungaji waliofanya hivyo kwa kuwalaghai waumini wao kwamba wana uwezo wa kufufua watu huku wakijua kwamba lengo lao ni kuwavutia watu wajazane kwenye makanisa yao ili wapate  sadaka nyingi,” kilisema chanzo chetu.

 Uchunguzi  umebaini  kwamba  kuna makanisa  ambayo  yana wafuasi wengi wa kufanya mazingaombwe ya namna hiyo na wamekuwa wakijipatia fedha nyingi ambapo kwa Jumapili moja, hujikusanyia kati ya shilingi 7,000,000 hadi 7,500,000.

Aidha, ‘hukomba’ sadaka wakati wa maombi ya katikati ya wiki kwa kutumia mbinu mbalimbali za kuvuta waumini.

Baadhi ya vijana wa kijiji hicho ambao  waliwahi kurubuniwa na wachungaji baada ya kufuatwa kijijini hapo ni pamoja na Ziada Mlanga (33) na Shakila Ayubu (29).
Katika  mahojiano  na mwandishi wetu kijijini hapo, Ziada alikuwa na haya ya kusema:
“Machi 21, 2011 kaka mmoja (jina tunalihifadhi) anayeishi Kijiji cha Makore jirani na chetu, alinifuata na kunieleza kwamba anahitaji vijana wanne, wa kike  wawili na wa kiume wawili ili wajiunge katika shughuli za sanaa, yaani kuigiza.

“Hata hivyo, alifanikiwa kunipata mimi na Shakila, akatuahidi kutulipa shilingi 350,000 kila mmoja na wazazi wetu kupewa shilingi 100,000 kila mmoja.

“Tulikubali  kufanya hivyo, walituchukua kwa pikipiki hadi Kijiji cha Makore  nyumbani kwa mtu mmoja aliyemtaja kuwa ni mchungaji.

“Tulipofika huko walituweka katika chumba maalum katika nyumba ya huyo mchungaji  ambayo ipo porini, wakatueleza kwamba  tusubiri kuna watu wanakuja kutupa  mafunzo.

“Baada ya muda mfupi walifika watu ambao tulipoongea nao, walitueleza tuvue nguo zote tubaki na za ndani. Tulifanya hivyo, wakatupaka majivu, wakatuvuruga nywele  na kutuvalisha nguo chakavu na ilipofika saa moja usiku, walikuja watu wengine wakiwa kwenye gari yenye vioo vya tinted.

“Walitueleza kwamba tunaelekea jijini Dar es Salaam ambako tukifika tujifanye mazezeta. Tulifika usiku sana na kupelekwa katika kanisa moja (jina linahifadhiwa).

“Ndani ya gari lile kulikuwa na bastola, hatukujua ni ya nini, pale kanisani tulitengenezewa chai. Hata hivyo, tulikataa  kuinywa.

“Baadaye walitueleza kwamba wametufanya vile ili tuonekane kama watu  waliokuwa wamechukuliwa kimazingara na kufanywa misukule na sasa tumeokolewa na mchungaji wa kanisa hilo.

“Kesho yake ilikuwa Jumapili, tuliambiwa tutasimama mbele ya waumini kanisani na tusiseme kitu chochote ili tuje kuanza kuongea kidogo baada ya kuombewa na mchungaji.

 “Hata hivyo, tulipewa majina ya watu mashuhuri waliokufa lakini mimi nilikataa kwa kuwa aliyetajwa kuwa nijifanye ndiyo mimi alikuwa mtu maarufu.

 “Nilijiuliza ndugu zake wangenielewaje? Kitu cha pili ni kwamba nilikataa kwa kuwa fedha tulizokubaliana walikuwa hawajatupatia na tukaona kuwa huo ni udhalilishaji.

“Baada ya kuona tumekataa, walitusihi  tusitoe siri na baadaye tulipewa nguo  nyingine tukavaa na tukapewa shilingi elfu hamsini kila mmoja kama nauli ya kurudia kijijini kwetu Kimange.

“Tulipofika tuliwaeleza wazazi wetu  mambo tuliyofanyiwa wakaona tumedhalilishwa, ikabidi tuje nao Dar es Salaam  tukaenda hadi Kituo cha Polisi  Magomeni na kufungua  kesi.

  “Tuliwaambia polisi kuwa simu na nguo zetu ziko kwa watu hao lakini hadi leo kesi tuliyofungua hatujui ilipofikia na tuliambiwa polisi wamewasiliana na wenzao wa Mkoa wa Pwani.

“Polisi wa Pwani walikuja Dar na kutuchukua hadi Kibaha ambako tulitoa maelezo na tukaenda nao Kijiji cha Makore lakini  hatukumkuta mchungaji huyo, tukaambiwa kuwa alihama baada ya kupata habari kuwa anatafutwa na polisi,” alisema Ziada akiungwa mkono na Shakila.


BABA  WA  ZIADA

Baba wa Ziada aliyejitambulisha kwa jina la Sijali Musini Mlanga, alisema kwamba kitendo walichofanyiwa watoto hao ni cha udhalilishaji na anaiomba serikali kuchukua hatua.

“Hatuwezi kukubaliana na hali hiyo, huo ni utapeli na udhalilishaji mkubwa, hakuna dini  inayoweza kufanya mambo kama hayo, wahusika wachukuliwe hatua,” alisema Mlanga.


MWENYEKITI  WA  KIJIJI

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimange, Juma Issa  Madinga amekiri kufahamu suala hilo na kukemea kitendo hicho.

“Hao wachungaji hawawezi kuachwa wakifanya mambo hayo na kusababisha kijiji kupakaziwa kuwa ni cha misukule, sasa wananchi wasilaghaiwe na matapeli hao, wakija tena watoe taarifa kwangu,” alisema  mwenyekiti huyo.

Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/04/kijiji-cha-misukule-chafumuliwa.html#ixzz2PIMQ5S1P

BOB JUNIOR awapagawisha wabongo DENMARK kwa show yake kali.

 

Monday, April 1, 2013

Maafa tena, kifusi chaua Arusha

 
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyepoteza maisha  kutokana na  kuporomoka kwa udongo katika machimbo ya Moramu yaliyopo eneo la Moshono, Arusha.  Picha na Filbert Rweyemamu 


 
Kwa ufupi
“Inasadikiwa kuwa zaidi ya wachimbaji 20 pamoja na magari mawili kwa ajili ya kubeba mzigo huo yalikuwapo ndani ya shimo hilo ambayo nayo yalifunikwa na kifusi hicho,”alisimulia Kamanda Kilonge.
Mussa Juma na Moses Mashalla, Mwananchi
Arusha. Siku tatu baada ya ghorofa kuanguka na kuua watu 36 jijini Dar es Salaam, maafa mengine yametokea jana mkoani Arusha ambako watu wapatao 20 wanahofiwa kufa baada ya kufunikwa na kifusi cha `moramu’ wakati wakifanya shughuli za uchimbaji eneo la Moshono, Arusha.

Maiti za watu 14 ndiyo zilikuwa zimeopoelewa hadi jana jioni wakati watu wawili tu ndiyo walikuwa wametoka wakiwa hai na kukimbizwa katika Hospitali ya Mt Meru kwa ajili ya matibabu kutokana na kuvunjika miguu.
Waliotolewa wakiwa hai walitambuliwa kuwa ni Matei Nenano na Lushooki Laizer wote wakazi wa jijini Arusha. Mwananchi lilishuhudia vikosi vya uokoaji kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi pamoja na wananchi wakitoa msaada wa kufukua kifusi hicho kwa ajili ya kutoa watu waliofunikwa.
Maiti zilizoopolewa ni za mmiliki wa magari ya kubeba kifusi hicho, Julius Peter, Alex Mariaki, Gerald Lutakata, Hassan Hamis, Sauli Raphael, Bariki Revelian na Kababuu Ruafela.

Wengine ni Mwenda Kiboliboli, Japhet Jivaline, Benard Masai, Gerald Jacob, Fredy Losileani, Julius Palangyo na mtu ambaye alijulikana kwa jina moja la Christopher.

Watu walioshuhudia tukio na taarifa hizo kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Hemed Kilonge walisema lilitokea jana saa 5.00 asubuhi wakati shughuli za uchimbaji zikiendelea.
Kamanda Kilonge alisema wakati wachimbaji hao wakiwa ndani ya shimo wakiendelea na kuchimba ‘moramu’, ghafla gema liliporomoka na kuwafunika.
Mashuhuda walisema wachimbaji hao walikuwa wakifanya shughuli zao huku mvua kubwa ikinyesha na kwamba kuna uwezekano hiyo ni sababu ya kuanguka kwa kifusi hicho.

Mvua ilikuwa ikiendelea hata wakati wa uokoaji, hali iliyofanya kazi hiyo kuwa ngumu.
“Inasadikiwa kuwa zaidi ya wachimbaji 20 pamoja na magari mawili kwa ajili ya kubeba mzigo huo yalikuwapo ndani ya shimo hilo ambayo nayo yalifunikwa na kifusi hicho,”alisimulia Kamanda Kilonge.
Uhaba wa mafuta
Mwananchi lilishuhudia magari ya uokoaji kutoka jijini Arusha yakiwa yameishiwa mafuta na kusababisha uokoaji kuzorota.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amelazimika kusitisha safari yake mkoani Tanga baada ya kupata taarifa ya tukio hilo na baadaye alitangaza kwamba Serikali imeamua kufunga machimbo yote ya `moramu’ hadi pale itakapotoa tamko lingine.
Akizungumza eneo la tukio, Mulongo alisema tukio hilo ni la kusikitisha kwa kuwa vijana waliokufa ni wengi.
Kwa upande wake mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema aliitaka Serikali kuweka utaratibu wa kukabiliana na matukio ya aina hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka viashiria vya usalama maeneo ya machimbo.

PICHA ZA UTENGENEZAJI WA VIDEO YA G NAKO 'MAMA YEYOO NA BEN POL ARUSHA

 

Kwenye picha ni Ben Pol,G Nako,Lord Eyes,Nisher na Ras Omega wakiwa ndani ya Maskani ya River Camp Soldier Arusha.
G Nako.
Nisher ambaye ndo Director wa Video hiyo
Ben Pol.

Fid Q, Stamina wagombania demu Coco Beach

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASANII wawili wa muziki wa Hip Hop nchini, Farid Qubanda Fid Q na Stamina, jana waliacha vituko katika Ufukwe wa Coco Beach, walipojionyesha dhahiri kuwa ni watu wa vitoto baada ya kujitoa mhanga na kuanza kugombania demu.
Stamina akifanya mashambulizi kwa ajili ya kumpata demu jukwaani. Ilikuwa balaa.
Hapa hawa wanafanyiwa usaili ili mmoja wapo atoke na mkali kati ya Fid na Stamina.
Demu aliyewatoa udenda Fid Q na Stamina akifurahia jukwaani.
Profesa Jay alikuwapo jukwaani katika tamasha la Vodacom Coco Beach
Afisa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, akiwajibika kwa kupiga picha jukwaani.

Vituko vya wasanii hao wanaotamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya vilianza baada ya kupanda jukwaani kuimba katika tamasha la wazi lililoandaliwa na Kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzania, kwa ajili ya kufurahia Sikukuu ya Pasaka na wateja wao.

Awali, Stamina ndio alikuwa wa kwanza kupanda stejini kuimba, lakini baadaye Fid Q naye alikwea jukwaani kumpa kampani mkali huyo, jambo ambalo lilianza kuibua hisia za wajamaa hao wanavyopenda watoto, yani wachumba.

"Jamani watu wanasema kuwa sisi hatuwezi kutongoza kama wanavyofanya wale wenzetu, sasa nataka mtupandishie kimwali kikali tuanze kusema nacho ili tuonyeshe kuwa nasisi tunayeweza kupita hata hao wengine wa Bongo Fleva,” alisema Fid Q na kuanza kuleta misuko suko kutokana na mashabiki kuanza kuwafanyia fujo watoto wa kike wakitaka wapande jukwaani.

Hata hivyo, baada ya kupanda wasichana wapatao watatu, mmoja alianza kuimbiwa mistari ya papo kwa papo kwa nia ya kumlainisha, jambo ambalo lilifanikisha kumuangukia Fid Q na kumtia kwapani na kushuka nay echini ya jukwaa.

Hata hivyo, staili hiyo ilikuwa ya kimasiahara tu kwa ajili ya kufurahia siku ya Pasaka, na hata kama aliondoka naye, hakuna ubaya hasa kama wenyewe watakuwa wameridhiana baada ya kuonana katika jukwaa hilo.

Tamasha hilo linaendelea leo katika fukwe hiyo ya Coco Beach ambapo burudani mbalimbali kutoka kwa wakali wa muziki nchini, akiwapo Afande Sele, Mashujaa Music na wengineo wamepangwa kutoa burudani.