Na Makongoro Oging', Bagamoyo
INATISHA na
hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi wa dini kuwatumia vijana wa
hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.
Uchunguzi
wa gazeti hili umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini kuteua kijiji
hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni kuwalaghai waumini
kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na kuchukuliwa
kimazingara.
Gazeti hili limebaini kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
Habari kutoka kijijini hapo zinadai kwamba viongozi wa dini wanaofika katika kijiji hicho wamekuwa wakiwalipa watu wanaojitokeza kuwa misukule bandia kati ya shilingi 200,000 hadi 250,000 kwa kila mtu.
Gazeti hili limebaini kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
Habari kutoka kijijini hapo zinadai kwamba viongozi wa dini wanaofika katika kijiji hicho wamekuwa wakiwalipa watu wanaojitokeza kuwa misukule bandia kati ya shilingi 200,000 hadi 250,000 kwa kila mtu.
Msukule.
Imegundulika kuwa viongozi hao wa dini hufanya zoezi hilo kwa siri
kubwa na kuna nyumba ya mchungaji mmoja, nje kidogo ya kijiji hicho
ambapo misukule hao feki hupewa mafunzo ya nini cha kufanya kabla ya
kusafirishwa kuelekea Dar es Saalam.
Imeelezwa kuwa misukule husafirishwa kwenye magari yenye vioo vyeusi
‘tinted’ wakiwa wamepakwa matope mwili mzima na kuvalishwa nguo
zilizochanika.
“Wapo wachungaji waliofanya hivyo kwa kuwalaghai waumini wao kwamba wana
uwezo wa kufufua watu huku wakijua kwamba lengo lao ni kuwavutia watu
wajazane kwenye makanisa yao ili wapate sadaka nyingi,” kilisema chanzo
chetu.
Uchunguzi umebaini kwamba kuna makanisa ambayo yana wafuasi wengi
wa kufanya mazingaombwe ya namna hiyo na wamekuwa wakijipatia fedha
nyingi ambapo kwa Jumapili moja, hujikusanyia kati ya shilingi 7,000,000
hadi 7,500,000.
Aidha, ‘hukomba’ sadaka wakati wa maombi ya katikati ya wiki kwa kutumia mbinu mbalimbali za kuvuta waumini.
Baadhi ya vijana wa kijiji hicho ambao waliwahi kurubuniwa na
wachungaji baada ya kufuatwa kijijini hapo ni pamoja na Ziada Mlanga
(33) na Shakila Ayubu (29).
Katika mahojiano na mwandishi wetu kijijini hapo, Ziada alikuwa na haya ya kusema:
“Machi 21, 2011 kaka mmoja (jina tunalihifadhi) anayeishi Kijiji cha
Makore jirani na chetu, alinifuata na kunieleza kwamba anahitaji vijana
wanne, wa kike wawili na wa kiume wawili ili wajiunge katika shughuli
za sanaa, yaani kuigiza.
“Hata hivyo, alifanikiwa kunipata mimi na Shakila, akatuahidi kutulipa
shilingi 350,000 kila mmoja na wazazi wetu kupewa shilingi 100,000 kila
mmoja.
“Tulikubali kufanya hivyo, walituchukua kwa pikipiki hadi Kijiji cha
Makore nyumbani kwa mtu mmoja aliyemtaja kuwa ni mchungaji.
“Tulipofika huko walituweka katika chumba maalum katika nyumba ya huyo
mchungaji ambayo ipo porini, wakatueleza kwamba tusubiri kuna watu
wanakuja kutupa mafunzo.
“Baada ya muda mfupi walifika watu ambao tulipoongea nao, walitueleza
tuvue nguo zote tubaki na za ndani. Tulifanya hivyo, wakatupaka majivu,
wakatuvuruga nywele na kutuvalisha nguo chakavu na ilipofika saa moja
usiku, walikuja watu wengine wakiwa kwenye gari yenye vioo vya tinted.
“Walitueleza kwamba tunaelekea jijini Dar es Salaam ambako tukifika
tujifanye mazezeta. Tulifika usiku sana na kupelekwa katika kanisa moja
(jina linahifadhiwa).
“Ndani ya gari lile kulikuwa na bastola, hatukujua ni ya nini, pale
kanisani tulitengenezewa chai. Hata hivyo, tulikataa kuinywa.
“Baadaye walitueleza kwamba wametufanya vile ili tuonekane kama watu
waliokuwa wamechukuliwa kimazingara na kufanywa misukule na sasa
tumeokolewa na mchungaji wa kanisa hilo.
“Kesho yake ilikuwa Jumapili, tuliambiwa tutasimama mbele ya waumini
kanisani na tusiseme kitu chochote ili tuje kuanza kuongea kidogo baada
ya kuombewa na mchungaji.
“Hata hivyo, tulipewa majina ya watu mashuhuri waliokufa lakini mimi
nilikataa kwa kuwa aliyetajwa kuwa nijifanye ndiyo mimi alikuwa mtu
maarufu.
“Nilijiuliza ndugu zake wangenielewaje? Kitu cha pili ni kwamba
nilikataa kwa kuwa fedha tulizokubaliana walikuwa hawajatupatia na
tukaona kuwa huo ni udhalilishaji.
“Baada ya kuona tumekataa, walitusihi tusitoe siri na baadaye tulipewa
nguo nyingine tukavaa na tukapewa shilingi elfu hamsini kila mmoja kama
nauli ya kurudia kijijini kwetu Kimange.
“Tulipofika tuliwaeleza wazazi wetu mambo tuliyofanyiwa wakaona
tumedhalilishwa, ikabidi tuje nao Dar es Salaam tukaenda hadi Kituo cha
Polisi Magomeni na kufungua kesi.
“Tuliwaambia polisi kuwa simu na nguo zetu ziko kwa watu hao lakini
hadi leo kesi tuliyofungua hatujui ilipofikia na tuliambiwa polisi
wamewasiliana na wenzao wa Mkoa wa Pwani.
“Polisi wa Pwani walikuja Dar na kutuchukua hadi Kibaha ambako tulitoa
maelezo na tukaenda nao Kijiji cha Makore lakini hatukumkuta mchungaji
huyo, tukaambiwa kuwa alihama baada ya kupata habari kuwa anatafutwa na
polisi,” alisema Ziada akiungwa mkono na Shakila.
BABA WA ZIADA
Baba wa Ziada aliyejitambulisha kwa jina la Sijali Musini Mlanga,
alisema kwamba kitendo walichofanyiwa watoto hao ni cha udhalilishaji na
anaiomba serikali kuchukua hatua.
“Hatuwezi kukubaliana na hali hiyo, huo ni utapeli na udhalilishaji
mkubwa, hakuna dini inayoweza kufanya mambo kama hayo, wahusika
wachukuliwe hatua,” alisema Mlanga.
MWENYEKITI WA KIJIJI
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimange, Juma Issa Madinga amekiri kufahamu suala hilo na kukemea kitendo hicho.
“Hao wachungaji hawawezi kuachwa wakifanya mambo hayo na kusababisha
kijiji kupakaziwa kuwa ni cha misukule, sasa wananchi wasilaghaiwe na
matapeli hao, wakija tena watoe taarifa kwangu,” alisema mwenyekiti
huyo.
Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/04/kijiji-cha-misukule-chafumuliwa.html#ixzz2PIMQ5S1P
0 comments:
Post a Comment