NOTE: Freestyle sio nguzo ya Hip Hop kama
wengi wanavyosema, ila freestyle iko ndani ya nguzo ya Hip Hop inayoitwa
Emceeing (Uchenguaji), ambapo mchenguaji anaweza akafanya mitindo huru.
Wengi wamekuwa wakizungumza kuwa kama mtu hajui ku-freestyle
basi sio MC, nakubaliana nao kabisa kwa sababu hakuna MC ambae hajui
kufreestyle na hajawahi kutokea, na hapa bongo pia hayupo. Lakini tunafahamu
maana halisi ya mitindo huru ama freestyle? Utakubaliana na mimi baada ya
kusoma dondoo hizi hadi mwisho.
Maana ya ‘freestyle halisia’
Katika kitabu kinachoitwa ‘How to Rap: The Art & Science
of Hip-Hop’, mwana HipHop mkongwe na mfatiliaji wa maswala ya Hip Hop anaeitwa
Big Daddy Kane, anaelezea kiundani kuwa freestyle halisia ni ile ya mashairi
yanayoandikwa kwanza kisha yanaimbwa lakini inakuwa free of style kwa sababu MC
hachaguliwi mada ya kuimba,anaandika kile anachotaka yeye kukiwakilisha katika
jamii.
Na hii ilikuwa ni mitindo huru iliyoshika chati sana miaka
ya 80, Kane anasema, “Miaka ya 80 tulipokuwa tukisema tunaandika mitindo huru
(freestyle), hiyo ilimaanisha ni mashairi uliyokuwa unaandika ambayo yalikuwa
‘free of style’...kimsingi ilikuwa ni mistari ambayo ulikuwa unajisifia na
kujikweza wewe mwenyewe.”
Mwanaharakati mwingine wa Hip Hop wa miaka hiyo anaeitwa Myke 9, nae aliongeza kwa kusema, “Miaka ile mitindo huru ilikuwa ni kuchana mistari kuhusu kitu chochote bila kupangiwa, na ilikuwa inaandikwa ama kukaririwa.”
Natika kitabu kingine kinachoitwa ‘There’s A God On The
Mic’, Kool Moe anaelezea maana ya
freestyle kama mistari iliyoandikwa ambayo mwandishi hachaguliwi mada ya
kuzungumzia.
Mfano mzuri, tukiangalia pia hata katika tuzo za hip hop
kama zile zinazotolewa na kituo cha runinga cha BET, BET HIP HOP AWARDS, Cypher
freestyle, wasanii wote huimba mashairi ambayo waliyaandika kabla ama
waliyakariri na hivyo wakati mwingine wenzao kufuatisha kile wanachoimba.
Freestyle ya mashairi
ya Kutoa kichwani papo kwa papo:
Haina maana kuwa mtindo huru wa kutoa mashairi kichwani sio
sahihi, lakini huu ni mtindo ambao umezaliwa kutoka katika mitindo huru ya
kuandikwa, na wakongwe katika Muziki wa Hip Hop wanasema mtindo huu ulianza
miaka ya 90, na uliitwa ‘off the top of the head’. Na hiki kilikuwa ni kipaji
kingine kabisa ambacho wengi walikikimbilia walikuwa hawana uwezo wa kuandika
mashairi mazuri, lakini wanaweza kutoa maneno kichwani na kuyapanga vizuri kwa
vina, hii baadae ilizaa freestyle battle (mashindano ya kughani kwa kutoa
mashairi kichwani papo kwa papo) ambayo ilivuma sana na kuwa burudani nyingine
katika vilinge (cypher).
Divine Styler anasema, “Katika shule niliyotokea, kufanya
mitindo huru ilikuwa ni kuimba mistari iliyoandikwa ambayo haina concept ya
kupangiwa.”
Mitindo huru ya Kutoa
Kichwani papo kwa papo ilianza lini?
Kool Moe ambae ni mkongwe na mfuatiliaji wa Hip Hop kwa
ukaribu sana anaeleza kuwa mitindo huru ya aina hii ya kutoa mashairi kichwani
papo kwa papo (off the top of the head), ilianza katikati ya miaka ya 80, na kushika kasi zaidi baada
ya Eminem kutoaa filamu ya 8’ Mile ambayo iliwahamashisha vijana wengi
kujiingiza katika aina hiyo ya mitindo huru.
“Hadi mwaka 1986, mitindo huru yote ilikuwa ni ya kuandika
mashairi kwanza ama kukariri, ilikuwa ni jinsi gani ungeweza kuja na mashairi
mazuri yaliyoandikwa bila kuwa na mada maalum na bila kuwa na sababu ya msingi
zaidi ya kuonesha uwezo wako ama ujuzi wako wa kuandika mashairi.”
Wapo wasanii wa hapa bongo wengi sana ambao ni wazuri sana
katika kufanya freestyle za kutoa kichwani kama God Zilla, Nikki Mbishi, Young
D, Ngwair na wengine wengi. Lakini wapo wengine ambao hawana kipaji cha kutoa
mashairi kichwani papo kwa papo lakini ni wakali sana hasa wakiandika mashairi,
hii haina maana kuwa kutokuwa na uwezo wa kutoa mashairi kichwani papo kwa papo
ni udhaifu katika Hip Hop.
MUCH RESPECT KWA JOSEFLY
CHANZO: www.leotainmenttz.com
0 comments:
Post a Comment