Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASANII
wawili wa muziki wa Hip Hop nchini, Farid Qubanda Fid Q na Stamina, jana
waliacha vituko katika Ufukwe wa Coco Beach, walipojionyesha dhahiri kuwa ni
watu wa vitoto baada ya kujitoa mhanga na kuanza kugombania demu.
Stamina akifanya
mashambulizi kwa ajili ya kumpata demu jukwaani. Ilikuwa balaa.Hapa hawa wanafanyiwa usaili ili mmoja wapo atoke na mkali kati ya Fid na Stamina.
Demu aliyewatoa udenda Fid Q na Stamina akifurahia jukwaani.
Profesa Jay alikuwapo jukwaani katika tamasha la Vodacom Coco Beach
Afisa
Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, akiwajibika kwa kupiga picha
jukwaani.
Vituko vya wasanii hao
wanaotamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya vilianza baada ya kupanda
jukwaani kuimba katika tamasha la wazi lililoandaliwa na Kampuni ya Simu za
Mikononi ya Vodacom Tanzania, kwa ajili ya kufurahia Sikukuu ya Pasaka na wateja
wao.
Awali,
Stamina ndio alikuwa wa kwanza kupanda stejini kuimba, lakini baadaye Fid Q naye
alikwea jukwaani kumpa kampani mkali huyo, jambo ambalo lilianza kuibua hisia za
wajamaa hao wanavyopenda watoto, yani wachumba.
"Jamani
watu wanasema kuwa sisi hatuwezi kutongoza kama wanavyofanya wale wenzetu, sasa
nataka mtupandishie kimwali kikali tuanze kusema nacho ili tuonyeshe kuwa nasisi
tunayeweza kupita hata hao wengine wa Bongo Fleva,” alisema Fid Q na kuanza
kuleta misuko suko kutokana na mashabiki kuanza kuwafanyia fujo watoto wa kike
wakitaka wapande jukwaani.
Hata
hivyo, baada ya kupanda wasichana wapatao watatu, mmoja alianza kuimbiwa mistari
ya papo kwa papo kwa nia ya kumlainisha, jambo ambalo lilifanikisha kumuangukia
Fid Q na kumtia kwapani na kushuka nay echini ya jukwaa.
Hata
hivyo, staili hiyo ilikuwa ya kimasiahara tu kwa ajili ya kufurahia siku ya
Pasaka, na hata kama aliondoka naye, hakuna ubaya hasa kama wenyewe watakuwa
wameridhiana baada ya kuonana katika jukwaa hilo.
Tamasha
hilo linaendelea leo katika fukwe hiyo ya Coco Beach ambapo burudani mbalimbali
kutoka kwa wakali wa muziki nchini, akiwapo Afande Sele, Mashujaa Music na
wengineo wamepangwa kutoa burudani.
0 comments:
Post a Comment