Kwa ufupi
“Inasadikiwa kuwa zaidi ya wachimbaji 20 pamoja na
magari mawili kwa ajili ya kubeba mzigo huo yalikuwapo ndani ya shimo
hilo ambayo nayo yalifunikwa na kifusi hicho,”alisimulia Kamanda
Kilonge.
Mussa Juma na Moses Mashalla, Mwananchi
Arusha. Siku tatu baada ya ghorofa kuanguka na kuua watu 36 jijini Dar es Salaam, maafa mengine yametokea jana mkoani Arusha ambako watu wapatao 20 wanahofiwa kufa baada ya kufunikwa na kifusi cha `moramu’ wakati wakifanya shughuli za uchimbaji eneo la Moshono, Arusha.

Maiti za watu 14 ndiyo zilikuwa zimeopoelewa hadi
jana jioni wakati watu wawili tu ndiyo walikuwa wametoka wakiwa hai na
kukimbizwa katika Hospitali ya Mt Meru kwa ajili ya matibabu kutokana na
kuvunjika miguu.
Waliotolewa wakiwa hai walitambuliwa kuwa ni Matei
Nenano na Lushooki Laizer wote wakazi wa jijini Arusha. Mwananchi
lilishuhudia vikosi vya uokoaji kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ), Polisi pamoja na wananchi wakitoa msaada wa kufukua kifusi hicho
kwa ajili ya kutoa watu waliofunikwa.
Maiti zilizoopolewa ni za mmiliki wa magari ya
kubeba kifusi hicho, Julius Peter, Alex Mariaki, Gerald Lutakata, Hassan
Hamis, Sauli Raphael, Bariki Revelian na Kababuu Ruafela.
Wengine ni Mwenda Kiboliboli, Japhet Jivaline, Benard Masai, Gerald Jacob, Fredy Losileani, Julius Palangyo na mtu ambaye alijulikana kwa jina moja la Christopher.
Wengine ni Mwenda Kiboliboli, Japhet Jivaline, Benard Masai, Gerald Jacob, Fredy Losileani, Julius Palangyo na mtu ambaye alijulikana kwa jina moja la Christopher.
Watu walioshuhudia tukio na taarifa hizo
kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Hemed Kilonge
walisema lilitokea jana saa 5.00 asubuhi wakati shughuli za uchimbaji
zikiendelea.
Kamanda Kilonge alisema wakati wachimbaji hao
wakiwa ndani ya shimo wakiendelea na kuchimba ‘moramu’, ghafla gema
liliporomoka na kuwafunika.
Mashuhuda walisema wachimbaji hao walikuwa
wakifanya shughuli zao huku mvua kubwa ikinyesha na kwamba kuna
uwezekano hiyo ni sababu ya kuanguka kwa kifusi hicho.
Mvua ilikuwa ikiendelea hata wakati wa uokoaji, hali iliyofanya kazi hiyo kuwa ngumu.
Mvua ilikuwa ikiendelea hata wakati wa uokoaji, hali iliyofanya kazi hiyo kuwa ngumu.
“Inasadikiwa kuwa zaidi ya wachimbaji 20 pamoja na
magari mawili kwa ajili ya kubeba mzigo huo yalikuwapo ndani ya shimo
hilo ambayo nayo yalifunikwa na kifusi hicho,”alisimulia Kamanda
Kilonge.
Uhaba wa mafuta
Mwananchi lilishuhudia magari ya uokoaji kutoka jijini Arusha yakiwa yameishiwa mafuta na kusababisha uokoaji kuzorota.
Mwananchi lilishuhudia magari ya uokoaji kutoka jijini Arusha yakiwa yameishiwa mafuta na kusababisha uokoaji kuzorota.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amelazimika
kusitisha safari yake mkoani Tanga baada ya kupata taarifa ya tukio
hilo na baadaye alitangaza kwamba Serikali imeamua kufunga machimbo yote
ya `moramu’ hadi pale itakapotoa tamko lingine.
Akizungumza eneo la tukio, Mulongo alisema tukio hilo ni la kusikitisha kwa kuwa vijana waliokufa ni wengi.
Kwa upande wake mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema aliitaka Serikali kuweka utaratibu wa kukabiliana na matukio ya
aina hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka viashiria vya usalama maeneo ya
machimbo.
0 comments:
Post a Comment