Blogger Widgets

Saturday, March 22, 2014

BAADA YA DOGO JANJA KUOMBA MSAMAHA NA KUTAKA KURUDI TIP TOP HII NDIYO KAULI YA BABA YAKE MZAZI JUU YA SWALA HILO..!!

Alhamisi ya March 20 2014 lilitoka tamko ambalo lina maamuzi ya msanii wa bongofleva Dogo Janja kuhusu kuomba msamaha na kuhitaji kurudi kwenye kundi lake za zamani la Tiptop connection na kuyasahau yaliyopita kati yake na aliyekuwa meneja wake pia ambae ni Madee.Stori hii ina pande nyingi sana ambazo zitazungumza kupitia hapahapa kwenye tovuti hii lakini kwa kuanzia, baba mzazi wa Dogo Janja amepata nafasi kuzungumza kwa mara ya kwanza baada ya mtoto wake kuomba msamaha.
Anasema >>’Dogo Janja alishakua mtu mzima na tayari nilishawahi kumwambia achague mahali atakapoona kuna manufaa kwake, akishafanya maamuzi yake huwa ananishirikisha kwenye kujadiliana, tayari alishawahi kuniambia kuwa atafanya maamuzi baada ya kuona Mtanashati hakuna muelekeo wowote na hakuna anachopata ndipo akaniambia baba mimi mtu yoyote au kundi lolote nitakalokubaliana nalo basi nitafanya nao kazi’.
Hayo ni maelezo ya Baba mzazi wa Dogo Janja ambae ametoa baraka zote kwa Janja kurudi kujiunga na Tiptop Connection hivyo kazi imebaki kusikia kutoka upande wa Tiptop kufahamu kama wameukubali msamaha wa Dogo Janja.

source: millard

1 comment:

  1. Wynn Casino in Las Vegas, NV - MapYRO
    Wynn Casino 강원도 출장마사지 in Las Vegas, NV. 3131 Las Vegas Boulevard South, Las Vegas, NV 진주 출장안마 89109 남양주 출장안마 - Use this 천안 출장마사지 simple form to find 사천 출장샵 hotels, motels,

    ReplyDelete