\
MWANAMITINDO wa kimataifa wa
Tanzania, Flaviana Matata ambaye ameng’ara kimataifa baaada ya kushinda
tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa mwanamitindo bora barani
Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).
MWANAMITINDO wa kimataifa wa
Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara kimataifa baaada ya
kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa mwanamitindo bora
barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).
Tuzo hiyo utolewa kwa
wanamitindo ambao bado wanailetea sifa Afrika kimataifa na Flaviana
amekuwa katika chati ya juu. Mwaka jana Desemba, Flaviana alishinda
tuzo nyingine ya uwanamintindo bora kutoka kwa diaspora ya Waafrika.
Flaviana kwa ambaye kwa sasa
anaishi na kufanya kazi ya uanamitindo New York nchini Marekani kupitia
shirika la Wilhelmina Models, mpaka sasa ameweza kuitangaza Tanzania
kimataifa kutokana na umahiri wake katika maonyesho ya mavazi.
Tangu ashinde taji la Miss
Universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana amekuwa aking’ara katika kona
zote za dunia na hasa baada ya kumaliza katika nafasi ya sita katika
mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, huku Tanzania ikishiriki kwa
mara ya kwanza.
Ameweza kushiriki katika
maonyesho ya mavaz mengi Ulaya na Amerika huku akitoa misaada mingi kwa
Watanzania wenzake ambao wamekuwa na ndoto ya kufika mbali katika fani
hiyo.
Kwa sasa Flaviana anaendesha
taasisi yake, Flaviana Matata Foundation ambayo inasomesha watoto wa
kike 16 na mwaka jana alitoa msaada wa vifaa vya kuokoa maisha kama
sehemu ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba huku ikiwa
kumbukumbu ya kifo cha mama yake mzazi katika ajali hiyo ya mwaka 1996.
Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni
ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria Sarungi Tsehai alisema
kuwa wamejisikia faraja sana kwa kumvumbua mwanamitindo huyo ambaye kwa
sasa anashika chati ya juu Tanzania na nje ya nchi.
Maria alisema kuwa Flaviana
amedhihirisha ubora wake na mpaka sasa amepitiliza kiwango cha
kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake, ndoto ambayo alikuwa nayo muda
mrefu.
0 comments:
Post a Comment