10:29 PM
RAISI
WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII,SANAA NA LUGHA CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM)
IDD MOHAMED NA WAZIRI WAKE WA FEDHA IBRAHIM MATATA WASHIKILIWA NA POLISI KWA
TUHUMA ZA WIZI WA SHILINGI MILIONI 15 NA LAKI 6,MALI YA SERIKALI YA WANAFUNZI WA
KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII,SANAA NA LUGHA CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA
(UDOM)
TAARIFA ZINASEMA
KUWA RAISI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII, SANAA NA LUGHA AMBAYE PIA NI
MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU ANAYESOMA BCOM ACCOUNTINGANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA
IDD MOHAMED ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KITUO CHA POLISI UDOM KWA TUHUMA ZA
WIZI WA FEDHA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 15 NA LAKI 6.
MTUHUMIWA
HUYO ALIKAMATWA JANA SIKU YA ALHAMISI AKIWA NA
MWENZAKE AMBAYE PIA ALIKUWA WAZIRI WA FEDHA WA KITIVO HIKO IBRAHIM MATATA AMBAYE
PIA NI MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU BCOM ACCOUNTING NA KUFIKISHWA KATIKA KITUO
HIKO CHA POLISI.
MARA
BAADA YA KUKAMATWA WALIKUTWA NA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 7 LAKI 2 NA 24
ELFU.(Shilingi 7,224,000 ZA Kitanzania.) Na fedha hizo zilitolewa kwenye account
ya serikali ya wanafunzi kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha na
kupelekwa katika Akaunti ya Mtu Binafsi ambaye ni Waziri wa Fedha wa Kitivo hiko
Ndugu Ibrahim Matata.
Chanzo hicho kiliendelea Kujuza kuwa Awali Raisi
Huyo Anahusika na kosa la kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni 1 na laki 1 katika
Duka lililopo Katika Bweni namba 13 (Block 13 ).
Raisi huyo pamoja na
Waziri wake wa Fedha walikamatwa Jana na kulala katika Kituo Cha Polisi Cha UDOM
tayari kwa Uchunguzi na hatua za kisheria Kuchukuliwa ili kuweza Kufikishwa
mahakamani
Habari zaidi ambazo Lukaza imezipata kutoka katika Vyanzo
vya habari Zinadai kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri wake Wa fedha watafikishwa
Mahakamani Jumatatu kwa tuhuma za wizi wa Shilingi Milioni 15 na laki 6 ambapo
waliweza kuzitoa na kuweka katika akaunti ya Waziri Wa Fedha Ibrahim Matata na
kufanikiwa kuchukua Sh Milioni 7 laki 2 na Ishirini na Nne elfu ambazo ndio
walikamatwa nazo Mkononi.
Hatimaye Bunge la Serikali ya Wanafunzi Wa
Kitivo Cha Sayansi ya Jamii ,Sanaa na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma
linatarajiwa kukaa leo Saa 10 Jioni ili kuweza kutoa uamuzi wa Kumvua madaraka
na kufikisha baadhi ya Ushaidi wa Sauti wakati Raisi huyo akiomba Rushwa katika
Duka lililopo Block 13.
0 comments:
Post a Comment