WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Hawa Ghasia amempasha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk
Hussein Mwinyi kuhusu ajira za madaktari akisema, wizara hiyo ina
utaratibu mbovu wa kuajiri unaowavunja moyo watumishi hao wa afya.
Ghasia na Mwinyi walitofautiana kuhusu suala hilo juzi kwenye kikao
cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii kilichofanyika Dar es
Salaam baada ya Dk Mwinyi kutoa taarifa ya wizara yake ambayo pamoja na
mambo mengine, ilieleza kuwapo mmoja wa madaktari wastaafu aliyeajiriwa
na kupewa cheo cha Mganga Mkuu wa Mkoa.
Katika taarifa yake zaidi, Dk Mwinyi alieleza kuwa kuna watumishi
ambao hupata mishahara bila kufanya kazi mkoani Manyara na kwenye Chuo
cha Mtapika, wakati pia kuna watoa huduma asilimia 50 waliopata mafunzo
lakini hawazingatii viwango vya kukinga na kudhibiti maambukizi katika
utoaji huduma za afya.
“Utunzaji wa dawa na vitendea kazi hauzingatii taratibu husika za
uhifadhi na uhakiki wa ubora wa vipimo vya maabara, kuna uagizaji wa
dawa nyingi kuliko mahitaji mkoani Mtwara, huduma zinazotolewa hazikidhi
matarajio ya wateja katika vituo vingi vya afya,”alisema Dk.
Mwinyi.
Ghasia
Baada ya kumaliza kusoma taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa kamati
hiyo chini ya mwenyekiti wao Dk Faustine Ndungulile, Ghasia alisema
baadhi ya matatizo kwenye wizara hiyo siyo ya msingi.
“Nina historia
yake huyo daktari alishawahi kufanya mambo ya ajabu tu hadi yakaripotiwa
kwenye vyombo vya habari sasa karudishwa na ndiye mganga mkuu, wakati
nikiwa utumishi nililipata hilo na nikashauri aondolewe kwenye nafasi
hiyo kwa kuwa hana sifa hiyo,” alisema.
Hatua hiyo ya Waziri, Ghasia ilitokana na taarifa aliyoiwasilisha Dk
Mwinyi kwa kamati hiyo aliyoeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2012/2013
wizara yake kupitia Idara ya Uhakiki na Ubora wa Huduma za Afya na
Ustawi wa Jamii imefanikiwa kufanya ukaguzi katika idara, taasisi na
vituo vya kutolea huduma vilivyopo chini ya wizara na kubaini kuna
upungufu mkubwa wa kiutendaji. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment