Dar es
Salaam
Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo ametangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa
Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili mwaka 2012, ambapo kiwango cha ufaulu
kimepanda kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 64.55 mwaka
2012.
Matokeo hayo
yametangazwa mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo
idadi ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 430,327, kati yao
wasichana walikuwa 205,476 na wavulana 224,851, ikiwa ni upungufu wa watahiniwa
36,240 ikilinganishwa na mwaka 2011 ambao walikuwa
466,567.
“Watahiniwa 386,271 sawa
na asilimia 89.76 ya waliosajiliwa, walifanya mtihani wakiwemo wasichana 187,244
na wavulana 199,027, watahiniwa 44,056 sawa na asilimia 10.24 hawakufanya
mtihani, kati yao wasichana ni 18,231 na wavulana 25,825” amesema
Mulugo.
0 comments:
Post a Comment