Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Sunday, September 23, 2012

‘ROSE NDAUKA’ AKAMILISHA FILAMU MBILI ‘UPOFU’ NA ‘SPECIAL COVER’…. KUZIACHIA OCTOBA…!!

 
MSANII mahiri anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu bongo Rose Ndauka, asema kuwa baada ya kuwa kambini kwa muda mrefu akitengeneza kazi ambazo awali alizitaja sasa zimekamilika na Octoba zinaenda sokoni ambazo ni ‘Upofu’ na ‘Special Cover’ huku zote zikiwa zimefanyika chini ya kampuni yake inayojulikana kama Ndauka Entertainment.

Awali msanii huyo alizungumza na DarTalk ambapo alisema kuwa filamu hizo zipo kwenye mchakato wa kupigwa picha lakini sasa ameamua kuweka wazi kuwa kila kitu kimekamilika na mwezi ujao zitakuwa sokoni kwa ajili ya kuwapa uhondo mashabiki.

Ndauka alisema kuwa ameamua kutoa filamu mbili kwa mpingo kwani mashabiki wake wana hamu ya kuona kazi nyingi zaidi na nzuri kutoka kwenye kampuni yake pia malengo yake ni kujitangaza zaidi kimataifa.

“Nakumbuka niliwahi kusema Octoba nitakuja na filamu mbili kutoka kwenye kampuni yangu kazi zipo tayari hivyo kinachosuburiwa ni ratiba ifike ili mashabiki wangu waweze kuona utamu wa kazi zangu, ujio huo utakuwa ni mzuri kwani utaifanya kampuni yangu iweze kujulikana zaidi kimataifa,” alisema. 

Maisha Plus 2012 usaili wa Dar

 Audition ya Maisha Plus hapa Dar ni Jumatatu kwenye attachment kuna full information.Kwa mliopo Dar, Team Maisha Plus inawaalika mfike Millenium Tower hiyo Jumatatu kuna mengi mazuri ya kushare nanyi kama familia yetu.



Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amelaani kitendo cha vyombo vya dola kuwapiga na kuwakamata wafuasi wa Cuf

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Shaif Hamad akizungumza na wahanga wa vurugu za uchaguzi mdogo wa Bububu huko ofisi kuu ya Chama hicho Mtendeni.
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Shaif Hamad akizungumza na wahanga wa vurugu za uchaguzi mdogo wa Bububu (hawapo pichani) huko ofisi kuu ya Chama hicho Mtendeni.
Mbunge wa Jimbo la Mtoni (CUF) Mhe. Faki Haji Makame akizungumza kwa niaba ya waganga wa vurugu za uchaguzi mdogo wa Bububu, mbele ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto). Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar.

Friday, September 21, 2012

MCHUNGAJI MSIGWA AENDELEZA VUGUVUGU LA MABADILIKO MKOANI IRINGA.

 Mbunge Peter Msigwa akiwa na viongozi wenzake wakati akiwahutubia wananchi Iringa eneo la soko kuu.

Umati wa wananchi uliofurika kumsikiliza

MBUNGE wa Iringa Mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Peter Msigwa jana ameongea na wananchi wake katika eneo la soko kuu la Iringa.

Thursday, September 20, 2012

HUYU NDIO MWANAMKE ALIOLEWA NA BABA MZAZI NA KUPATA WATOTO BILA KUGUNDUA.

Add caption
Taarifa ambayo imewashtua watu wengi inamuhusu mwanamama Valerie Spruill ambae ameishi na baba yake mzazi kama mke na mume kwa miaka 40 bila kugundua.
kwa mujibu wa Daily Post Nigeria, Spruill aligundua hii siri mwaka 2004 na amewavutia wengi kwa ujasiri wake wa kuiweka wazi kuhusu mumewe ambae kwa sasa ni marehemu.
Chanzo cha yeye kufahamu ni kutokana na kukusanya taarifa mbalimbali ambazo mwanzoni alianza kuzipata kama tetesi za umbea kutoka kwa watu mbalimbali.
Mpaka sasa mama huyu mwenye umri wa miaka 60 ana watoto watatu na wajukuu nane na alifahamu ukweli wa hii ishu kupitia kwa Uncle wake siku chache baada ya kifo cha mume wake.
Umeshawahi kusikia kisa cha aina hii? unemfahamu yeyote? mawazo yako ni yapi ili kuepuka vitu kama hivi? share na mimi kwa kucomment mtu wangu wa nguvu.

Wednesday, September 19, 2012

AJALI MBAYA MKOANI MBEYA: KAMBA YA KUFUNGIA NG'OMBE PAMOJA NA GOGO LA MTI VYATUMIKA KUFUNGIA USUKANI WA BASI LA ABIRIA.



 Sehemu ya chini ya usukani ukiwa umefungwa kwa kamba (ambayo hutumika kufungia ng'ombe) na mti kama uonavyo pichani,katika basi la abiria linalomilikiwa na Kampuni la Mwasha ambalo husafirisha

Tuesday, September 18, 2012

KAMA UMEZALIWA HI LEO UTAKUA UMEZALIWA NA STAR HUU.

MSANII ANAEKIMBIZA KWA STYLE YAKE YA RAGA A. TOWN YUNG OMEGA AMEZALIWA TAREHE 18/09/1992, HII LEO AMETIMIZA MIAKA 20 AMEONGEA NA BLOG HII the HOOD infotainment  ANAFURAHI SANA KUTIMIZA MIAKA HII NA ANAMSHUKURU MUNGU PAMOJA NA MAMA YAKE MZAZI KWA KUMLINDA KWA KIPINDI CHOTE TANGU AMEKUJA DUNIANI HADI HIVI SASA. VILEVILE ANAWAOMBA MASHABIKI WAKE WAENDELEE KUMPA SUPPORT YAKUTOSHA NA WAMUOMBEE KWA MUNGU AENDELEE KUFANYA VIZURI KWENYE HII GAME.

the HOOD infotainment INAKUTAKIA MAISHA MAREFU NA MUNGU AKUJALIE HERI NA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO YA MUZUKI NA MAISHA YA KILA SIKU.
 

Monday, September 17, 2012

Usaili video ya Diamond Nyumbani Lounge

diamond
USAILI wa wanamitindo na wachezaji watakaonekana kwenye video mpya ya msanii wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Kinondoni, Dar es Salaam.

Saturday, September 15, 2012

WADANGANYA NA KUJIPATIA FEDHA KWA JINA LA ASHA ROSE MIGIRO

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Wakala wa kupakia na kupakua mizigo bandarini ya Mokha Agency Co. Ltd, Mohamed Lema akionesha Taarifa ya Polisi (RB) kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo waliyofungua katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi baada ya watu waliofahamika kwa majina ya Yusuf Kalala na mke wake Sharifa Kalala kuitapeli kampuni hiyo kiasi cha fedha shilingi milioni 11.1 kwa kujipatia huduma kwa njia ya udanganyifu wakutumia jina la aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Katikati ni Msemaji wa kampuni hiyo, Salim Dawa na mmoja wa wanafamilia hiyo, Amin Kulateni.

TAHADHARI DHIDI YA MVUA ZA OKTOBA 2012–DISEMBA, 2012


 Kufuatia Utabiri wa Hali ya Hewa uliofanywa kwa pamoja na Mamlaka za Hali ya Hewa kwa nchi za Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki, Mamlaka ya Hali ya Hewa – Tanzania imetoa taarifa kuhusu uwezekano wa nchi kupata mvua nyingi iliyo juu ya wastani. Hali hii ya kuwa na mvua nyingi inatabiriwa kuikumba nchi kwa kipindi cha Oktoba, 2012 hadi Disemba, 2012 na huenda ikaendelea zaidi.

Hii ndio maana ya neno BADO NGWARE "G-NAKO"

Pichani: G-Nako & Nikki wa Pili
 
Msanii kutoka kundi la Weusi G-Nako ametiririka na Bongo Star Link na kusema maana ya neno BADO NGWARE ambapo jina hili amelitumia katika track zake mbili ile ya kwanza aliyomshirikisha Peter Msechu na hii rmx ambayo kamshirikisha Nikki wa Pili. 
G-Nako anasema maana ya neno hilo ni BADO MAPEMA na kama unataka kujua maneno yaliyosemwa humo ndani isikilize track hii ambayo ni remix

Friday, September 14, 2012

USAILI WA MAISHA PLUS 2012 UNAENDELEA MIKOANI

                          Hii ndiyo team nzima ya maisha plus inayofanya usaili mikoani kote Tanzania.

KILICHOIKUTA KAMATI ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA KIFO CHA MWANDISHI IRINGA.

 
  
 
Ikiwa ni siku moja tu baada ya kufikishwa Mahakamani kwa askari polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya mwandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi,