diamond
USAILI wa wanamitindo na wachezaji watakaonekana
kwenye video mpya ya msanii wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond
Platnumz’ unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Kinondoni,
Dar es Salaam.
Akizungumza mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Kampuni One Touch Solutions, Petter Mwendapole amesema wamechagua Nyumbani
Lounge kwa kuwa ni rahisi kufikika na watu wengi kwa urahisi.
“Mchujo wa wale watakaotaka kushiriki kwenye video
hiyo mpya ya Diamond Platnumz itafanyika nyumbani, kuna mambo mengi pia
yamechangia katika kufanya usaili huo Nyumbani.
“Nyumbani lounge inamilikiwa na msanii mwingine wa
kimataifa wa Tanzania Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’, na huyu ni msanii wa
kwanza kuweza kusimama mwenyewe na kujitegemea, mchango wake ni mkubwa katika
ulimwengu wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, wanaohitajika kuja kwenye usaili
pia tunatarajia watakuja kujitegemea kwa kuafata nyayo za JD,” alisema.
Mwendapole alisema, uongozi wa Nyumbani Lounge
chini ya Mkurugenzi wake Gadner G Habash ulipopewa wazo la kufanyika usaili huo
hawakusita na walipokea kwa mikono miwili na kuahidi kushirikiana na timu nzima
ya Diamond katika kuhakikisha usaili huo unafanikiwa.
Mkurugenzi huyo pia alisema watu wengi wamekuwa wakiuliza
maswali kuhusu malipo na vigezo ambavyo vitatumika katika kuwapata watu
watakaoshiriki kwenye usaili huo ambapo alieleza kuwa watakaochaguliwa
watalipwa na ndio maana kumewekwa usaili.
“Wote watakaochaguliwa kuonekana kwenye video hiyo
watalipwa, mpango wa Diamond ni kutengeneza ajira kwa watu wengine si kuuza
sura kama watu wengi wanavyowaita wale wanaonekana kwenye video, vigezo pale
kutakuwa wabunifu wa mitindo ambao wamesomea kazi zao, kutakuwa na walimu wa
muziki, kutakuwa na watu ambao wamesomea mambo ya uongozaji wa picha na
kurekodi, hii timu itaangalia vitu vingi kupata washindi,” alisema.
Alisema washiriki wanatakiwa kuja na nguo za
kuogelea, kutokea, ambapo pia kutakuwa na Red Carpet. Hii ni mara ya kwanza kwa
watu wanaotakiwa kuonekana kwenye video kufanyiwa usaili.
0 comments:
Post a Comment