Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Sunday, June 9, 2013

ANGALIA PICHA ZA WASANII NA LIST NZIMA YA WASHINDA WA TUZO ZA KILIMANJARO AWARDS 2013


Usiku wa tuzo za KTMA ulipambwa na burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Linah, Amini, Richie Mavoko, Mataluma, Hussein Jumbe, Zahir Zorro, Patricia Hillary na Barnaba. Wengine ni Snura, Godzilla, Mabeste, Madee na Afande Sele.
Host wa tuzo hizo mwaka huu alikuwa ni Zembwele na TJ.

Hii ni list nzima ya tuzo hizo.

Wimbo bora wa mwaka
Dear God – Kala Jeremiah

Msanii bora wa Kiume
Diamond

Msanii bora wa kike 
Lady Jaydee

Msanii bora wa kike Taarab
Isha Mashauzi

Msanii bora wa kiume Taarab
Mzee Yusuf

Msanii bora wa kiume Bongo Flava
Diamond

Msanii bora wa kike Bongo Flava 
Recho

Msanii bora wa Hip Hop
Kala Jeremiah

Msanii bora wa kiume Bendi
Chalz Baba

Msanii bora wa kike Bendi
Luiza Mbutu

Msanii bora anayechipukia
Ally Nipishe
Video bora ya mwaka
Baadaye – Ommy Dimpoz

Mtunzi bora wa mashairi Taarab
Mzee Yusuf

Mtunzi bora wa mashairi Bongo Flava
Ben Pol

Mtunzi bora wa mashairi hip hop 
Kala Jeremiah

Mtunzi bora wa mashairi Bendi
Chalz Baba

Mtayarishaji bora wa mashairi muziki wa kizazi kipya
Man Walter

Mtayarishaji wa wimbo wa mwaka – Taarab
Enrico

Mtayarishaji wa wimbo mwaka – Bendi
Amoroso

Mtayarishaji chipukizi wa mwaka
Mesen Selekta
Rapper bora wa bendi
Fagasoni

Wimbo bora wenye vionjo vya asili
Chocheeni Kuni – Mrisho Mpoto ft Ditto

Wimbo bora wa bendi
Risasi Kidole – Mashujaa Band

Wimbo bora wa Reggae
Kilimanjaro – Warriors from The East

Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Valu Valu – Jose Chameleone

Wimbo bora wa Bongo Pop
Me an You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee

Wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa
Me and You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee

Wimbo bora wa Hip Hop
Nasema Nao – Nay wa Mitego

Wimbo bora wa rnb
Kuwa na Subira – Rama Dee ft. Mapacha

Wimbo bora wa ragga/ dancehall
Predator – Dabo

Wimbo bora wa Taarab 
Mjini Chuo Kikuu – Khadija Kopa

Wimbo bora wa zouk rhumba 
Ni wewe – Amini

Bendi bora ya mwaka
Mashujaa Band

Kikundi bora cha Taarab 
Jahazi Modern Taarab

Kikundi bora cha muziki wa Kizazi kipya
Jambo Squad
Hall of Fame – Institution
Kilimanjaro Band wana Njenje

Hall of Fame – Individual
Salum Abdallah





KIFO CHA ALBERT MANGWEA – HIVI UNADHANI KIFO CHAKE KINATUULIZA MASWALI GANI ?.


Albert Mangwair PerformingNa Freddy Macha.
BABU wa fasihi ya Kiswahili, Shaaban Robert alifariki mwezi huu mwaka 1962. Ingetakiwa sikukuu ya kifo chake yaani Juni 20 ifanyiwe maadhimisho kila mwaka. Sisi na wenzangu wa Bendi ya Sayari tuliwahi kusheherekea kwa maonyesho ya 1983. Hazina hii tukufu ya taifa inatakiwa zaidi ya hilo.

Moja ya vitabu vyake babu ni “Kielezo cha Fasili” kilitolewa upya na mwongozi wa wachapishaji Tanzania; “Mkuki na Nyota” ,2004 na kinafafanua mashairi yake kwa wasomaji mintaarafu ya kujenga mapafu kilugha.

Ananyambua Shairi la “Jina”: “Mwanadamu mwenye fikra njema huacha fahari au sifa kwa wat
u ambayo vizazi vyake vya nyuma yake hupenda kuiona na ambayo itakuwa kama hazina kwa watu wote katika dunia.”

Albert Mangwea hakuwa Shaaban Robert; amefariki akiwa na miaka 31 tu. Lakini Mangwea au Mangair alitumia fani ya ushairi kuchangia kuiendeleza fasihi ya Kiswahili na kipaji chake alichomegewa na Muumba.

Kifo hiki kilichokua Usauzi (Afrika Kusini) kimezungumziwa na kinaendelea kuzungumziwa. Mwaka jana wakati kama huu, Tanzania ilimpoteza Steve Kanumba. Vifo vya chipukizi hawa vimeacha utata na mijadala marefu.

Mangwea alifia ughaibuni. 
Maisha ugenini ni magumu maana habari huwa hazitangazwi sana. Mbali na taratibu za kisheria, kinachongojewa kutufariji huwa viongozi wa dini na Serikali.

Vipo vifo vya aina nyingi. Ila vifo vinapokuwa na utata husubiri mkono wa sheria utubembeleze. Kanumba alifuatiliwa na mashtaka ya msichana aliyekuwa naye; Mangwea, hatuyajui bado kiuhakika...

Miaka iliyopita habari za vifo vya Waafrika hasa zile zilizohusiana na Ukimwi au dawa za kulevya hazikuwekwa wazi, sababu ya aibu, miiko na staha. Nakumbuka wanamuziki wawili maarufu Hukwe Zawose na mpwa wake, Charles Zawose walipofariki, wanahabari hatukueleza chanzo ili kuheshimu hisia za familia zao.

Magazeti ya ughaibuni, walakini, hayakupepesa.

Mwanamuziki Charles Zawose alifariki ghafla akijitayarisha kupanda ndege Sweden alikokuwa akifanya maonyesho ya muziki wa kijadi, 2004. Kwa kuwa Charles na baba yake mkubwa walishajenga majina ugenini habari zilichambuliwa katika magazeti viongozi. Mwandishi John Lusk wa “Independent” gazeti linaloheshimika sana Uingereza aliandika:

“Kifo kimenyamazisha moja ya himaya kubwa ya familia ya wanamuziki wa Tanzania... Walikuwa mabalozi viongozi wa muziki wa Kigogo.” Akaongeza kuwa Zawose amefariki kutokana na “maradhi yaliyosababishwa na Ukimwi.”

Nyumbani, lakini, ugonjwa haukutajwa.
CHANZO MWANANCHI.

Saturday, June 8, 2013

MAMBO MAKUU 5 YA KUSHANGAZA WAKATI WA MAZISHI YA NGWEA..!!

 

HUKU Albert Kenneth Mangwea ‘Ngwea’ akiwa kaburini siku ya pili leo kufuatia kufariki dunia ghafla usingizini nchini Afrika Kusini, Mei 28, mwaka huu, mambo matano ya kushangaza yamezuka katika kipindi chote cha msiba, Risasi Jumamosi linakupa kila kitu. 
Kwa mujibu wa utafiti wetu wa kina, waombolezaji mbalimbali wamekuwa wakiyazungumzia mambo hayo huku wengine wakihoji kuwepo kwake.


1. RIPOTI YAFICHWA KIBINDONI

Usiku wa kuamkia mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kihonda, Morogoro, paparazi wetu alipata bahati ya kuzungumza na mama wa marehemu Ngwea, Denisia Mangweha.
Katika mazungumzo hayo, mwanahabari wetu alimuuliza mama huyo kama alikuwa amekabidhiwa ripoti ya daktari inayotatua fumbo la nini kilimuua Ngwea.

Haya hapa majibu ya mama huyo:
“Sijapata wala sijui chochote kuhusu hiyo ripoti, wala sijui nani anayo.”
Jumanne iliyopita, ilidaiwa kuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo aliyekuwa ‘Sauzi’ ndiye aliyekabidhiwa ripoti hiyo ambapo na yeye aliikabidhi kwa ndugu wa marehemu. 
Kwa kawaida, ripoti inayoweka wazi kiini cha kifo cha marehemu husomwa siku ya mazishi, jambo ambalo halikufanyika siku ya kumzika Ngwea.
MANENO YA WATU MAKABURINI
Baadhi ya waombolezaji waliokuwa makaburini hapo, walitoa hisia zao wakidai kwamba, inawezekana ripoti hiyo haikuwa nzuri hivyo ili kulinda heshima ya marehemu ililazimika kuiacha kibindoni.
2. MAMA WA MAREHEMU AMTAMBUA DEMU MZUNGU
Jumatano, siku moja kabla ya mazishi, mama wa marehemu alimshika mkono aliyekuwa mchumba wa marehemu, yule mwanamke Mzungu akisema Albert (Ngwea) alikuwa akienda naye nyumbani hapo (Morogoro).
Alisema mara kadhaa walitoka yeye, marehemu na Mzungu huyo kwenda kula ‘bata’ mahali kabla ya kurejea Dar. Kwa hiyo Mzungu ni mwanamke aliyekuwa akitambulika na mama wa marehemu.
Cha kushangaza, dada wa marehemu aitwaye Neema Mangweha, alisema mchumba wa marehemu anayemjua yeye anaitwa Siwema ambaye kwa sasa ana ujauzito wa mwanamuziki maarufu wa muziki wa kizazi kipya Bongo.
3. MTOTO WA MAREHEMU AIBUKIA MAKABURINI
Alhamisi, wakati msafara wenye mwili wa marehemu ukiwa makaburini, mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Paulina Jeremiah akiwa na mtoto wa kike alijitokeza hadharani na kukutana uso kwa uso na paparazi wetu akidai mtoto huyo ni wa marehemu Ngwea.
Mwanamke huyo, mkazi wa Kigamboni, Dodoma alisema mtoto huyo anaitwa Neema Albert, alimzaa mwaka 2001 wakati huo Ngwea alikuwa akisoma Sekondari ya Mazengo.
Wakati anajieleza hayo, ndugu wawili wa marehemu walitokea, mmoja akiitwa Anthony Kenneth Mangweha na kumsikiliza mama Neema.
Anthony alimuuliza mama Neema kama kuna ndugu yeyote wa marehemu anayetambua uwepo wa mtoto huyo, mama Neema akawataja.
Aliwataja vijana watatu kwa jina mojamoja, Frank, Jotam na Amani ambapo alisema waliwahi kutumwa na marehemu kwenda Dodoma kumwangalia mtoto huyo.
Anthony alikiri kuwa vijana hao watatu ni ndugu wa familia hiyo na akamtaka mama Neema kupoa, baada ya mazishi na kurudi nyumbani watakaa kuzungumzia suala hilo.
4. M 2 THE P AIBUKIA KWENYE KUAGA MWILI
Katika hali iliyowashangaza wengi, msanii wa Bongo Fleva aliyepata matatizo na marehemu lakini yeye akapona, Mgaza Pembe ‘M 2 THE P’ aliibuka kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambako mwili wa marehemu ulikuwa ukiagwa.
Baadhi ya watu waliomtambua msanii huyo walionekana kumshangaa sana huku wakihoji ametua lini kutoka Sauzi.
M 2 The P alishindwa kuhimili wakati anapita kwenye mwili wa marehemu, alimwaga machozi, hali iliyosababisha waombolezaji wawili kumshika kulia na kushoto na kumtoa eneo hilo. 

MAVAZI YAKE SASA!
Kikubwa kilichoibua maswali kutoka kwa waombolezaji ni jinsi msanii huyo alivyovaa. Wengine waliamini vaa yake ilisababishwa na kutaka kujificha watu wasimtambue. Pia wapo waliodai inawezekana alitoroka huko Sauzi.
Alivaa suruali ya ‘jinzi’, fulana ya mikono mifupi, miwani na kofia kubwa licha ya 
hali ya hewa Morogoro kuwa si ya baridi sana kiasi cha kuvaa hivyo.
5. KUMBE MAREHEMU ALITUMIWA FEDHA SAUZI
Tofauti na mashabiki wake walivyoamini kuwa marehemu alikuwa akipiga fedha ndefu Sauzi na kuzituma Bongo kwa wanafamilia, mmoja wa ndugu zake alibumburua siri kuwa kuna wakati hali ilikuwa mbaya hadi ikabidi amtumie shilingi laki moja na nusu.
“Watu wanadhani labda Albert (Ngwea) alikuwa mambo safi muda wote Afrika Kusini kama vijana wengi wanavyoamini. Si kweli kuna wakati kabisa alikuwa akinipigia na kuniambia hali ilivyokuwa mbaya,” alisema ndugu huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.

ANGALIA HAPA "LIVE" MATUKIO YOTE YANAYOENDELEA HIVI KILI MUSIC AWARDS 2013

fungua link hiyo hapo chini uangalie LIVE matukio yote yanayoendelea hivi sasa kuhusu KILI MUSIC AWARDS
 http://new.livestream.com/KTMA2013

Thursday, June 6, 2013

Picha 5 za Ushahidi wa msanii M2theP kuhudhuria mazishi ya Marehemu Ngwea

.
.
.
.
.
.
.
.
.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA MILLARD AYO
.

MAREKANI YAUNDA SHERIA KUWADHIBITI WANAUME WANAOVAA SURUALI CHINI YA MAKALIO YAO

Sina shaka umeshasikia style za uvaaji wa suruali hususan kwa wanaume zenye majina kama mlegezo au kata k, au yawezekana ukawa huzijui kwa majina lakini umeshashuhudia vijana wamevaa suruali chini ya makalio.
Kama ambavyo mabinti wamekuwa wakilaumiwa kwa mavazi ya kuonyesha miili yao hasa sehemu nyeti, na upande wa wanaume wamekuwa wakilalamikiwa kwa style hiyo ya uvaaji ambayo imeonekana kuigwa hata na vijana wadogo ambao bado wako shuleni.
Katika hali ya kukerwa na tabia ya vijana kuvaa suruali chini ya makalio uongozi wa Wildwood, New Jersey nchini Marekani umeandaa sheria mpya itakayoweza kuwadhibiti wale wote wenye tabia hiyo ya kuvaa mlegezo na kukatiza mitaani.
Sheria hiyo inaelekeza wavaaji wote wa suruali, kaptura, mavazi ya kuogelea na sketi zisivaliwe chini ya inchi 3 kutoka kiunoni mwa mvaaji.
Mayor wa Wildwood Ernie Troiano Jr. aliwaambia waandishi wa habari kuwa amechoshwa na malalamiko anayoyapata juu ya vijana wanaotembea makalio nje kwa kushusha suruali zao kupita kiasi.
Unaonaje sheria kama hii ikija Tanzania pia?

TUSIPOCHUKUA HATUA, DAWA ZA KULEVYA ZITAWAMALIZA WANAMICHEZO NA WANAMUZIKI WA TANZANIA

DAWA za kulevya ni hatari, ni hatari sana. Maisha ya baadhi ya wasanii na wachezaji yamepotea kutokana na matumizi ya dawa hizo.Aidha, dawa za kulevya husababisha baadhi ya wasanii na wachezaji kushindwa kuendelea na fani zao.
Orodha ya wasanii waliopoteza maisha kutokana na matumizi ya dawa za kulevya ni ndefu lakini baadhi yao ni Elvis Presley, Whitney Houston, Brenda Fassie wa Afrika Kusini.

Tanzania imepata mshtuko kwamba kimeripotiwa kifo cha msanii kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Tukiwa tunangoja ripoti kamili ya daktari juu ya kifo chake, msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’, Albert Mangwea ‘Mangwair au Ngwea’ anadaiwa kufariki kutokana na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini mapema wiki iliyopita.

Habari hizo ziwe kweli au la, Mangwair amefariki na mwili wake ulirejeshwa nchini juzi kwa mazishi yaliyofanyika jana huko Morogoro. Hata hivyo kifo chake, kitoe changamoto kwa wasanii wengine  akiwemo Ray C aliyeko kwenye kituo cha kujirekebisha kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.


DAWA ZA KULEVYA
 
Hizi ni dawa ambazo zimepigwa marufuku kutumiwa na jamii kutokana na kiwango chake cha athari kwa binadamu. Dawa hizi ambazo miongoni mwake ni bangi, heroin na cocaine, zina athari zaidi katika mwili wa binadamu kuliko faida.

Wasanii wanaotumia dawa za kulevya husukumwa zaidi na tabia ya kuiga ili waweze kufanya maonyesho jukwaani kwa ukakamavu mkubwa.

Wasanii hawa wanaamini wanapotumia dawa hizo zinawasisimua mwili ili wapate uwezo wa kutumbuiza jukwaani kwa muda mrefu bila kuchoka tena bila aibu.

Upande wa wanamichezo hasa soka na riadha, msukumo mkubwa upo katika kuwa na pumzi ya kuweza kucheza soka kwa dakika 90 bila kuchoka na moyo wa ujasiri hata kwenye riadha hali ni hivyo hivyo.

ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYA MICHEZONI

Serikali duniani kote zinapiga marufuku matumizi ya dawa za kulevya. Kwa bahati mbaya, dawa hizi hutengenezwa, husafirishwa na hutumiwa kwa kificho japokuwa madhara hujionyesha wazi.

Kwa mujibu wa wataalam, mtu anapotumia dawa za kulevya, moja kwa moja huathiri baadhi ya viungo vya mwili kinyume cha imani ya watumiaji.

Mtumiaji hupata ganzi na kutoka katika hali ya kawaida. Kutokana na ganzi hiyo taarifa hutumwa katika ubongo na ubongo nao hutuma vichocheo katika kiungo hicho na hufanya kazi maradufu.

Jinsi dawa inavyotumiwa kwa wingi ili kurekebisha hali ya ganzi ndivyo nguvu inavyozidi kutengenezwa na hivyo ndivyo vinavyowamaliza wasanii na wanamichezo.

Wataalam wanasema matumizi haya ya dawa za kulevya huufanya mwili wa mtumiaji kuchoka na kukosa hamu ya kula kutokana na seli nyingi mwilini kushindwa kufanya kazi.

Matokeo yake, mwili wa mtu huyo hudhoofu kwa kukosa chakula na hata uwezo wa kutengeneza chembechembe hai za kuulinda mwili na kujikinga dhidi ya magonjwa hupungua, hivyo mwili huruhusu magonjwa ya mara kwa mara.

Hali hii inapotokea uwezo wa msanii au mwanamichezo huonekana umepungua na muda wowote mahala popote anaweza kuchukua maamuzi anayoyajua yeye.

KITU CHA KUFANYA

Masomo ya dini za Kikristo na Kiislamu na elimu maalum ya dawa za kulevya yatumike ili kuwaweka vijana katika misingi mizuri ya maadili na athari za dawa za kulevya.

Hii itasaidia vijana kufahamu kwa undani faida za dawa zilizoidhinishwa na Serikali na athari za dawa zilizopigwa marufuku zikiwemo za kulevya ili kupunguza kwa wimbi la vijana kutumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya.

MAKALA HII IMETOLEWA KATIKA GAZETI LA MAWIO NA IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI

ANGALIA PICHA ZA MAMBO YA WALIMWENGU


ANGALIA PICHA ZA MBUNGE SUGU NAYE WASHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU MANGWEA

 Mbunge Sugu anamuaga Ngwair katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Hapa jeneza la Ngwair linaingizwa karubini, ikiwa ni picha inayoonyesha kuwa hatutaweza tena kukutana na msanii huyu hapa chini ya jua. R.I.P Ngwair.....MAELFU ya watu walijazana leo katika Mkoa huu wa Morogoro kwa ajili ya mazishi ya msanii Albert Mangweha Ngwair, huku aliyepata naye matatizo nchini Afrika Kusini, Mgaza Pembe M to The P naye akiwa miongoni mwa waliohudhuria mazishi ya Ngwair.
 Hapa M to The P akilia baada ya kupita kwenye jeneza la Ngwair katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika Kihonda Kanisani jioni yake.
Mama wa Ngwair akizungumza na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Joel Bendera, leo mjini Morogoro, kabla ya mazishi ya msanii huyo wa Hip Hop Tanzania

Mwili wa Ngwair unaingizwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Hapa watu wanakanyagana kwa ajili ya kujipanga mstari kwenda kumuaga marehemu Ngwair, leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ulikuwa umejaa watu, sambamba na wale waliojipanga barabarani kwa ajili ya kuangalia msafara wa Ngwair uliofunika mji wote siku ya leo.

Tukio la kuzikwa lilitanguliwa na shughuli ya uagaji iliyofanyika pia katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, baada ya kuona mkanyagano wa watu wengi nyumbani, usiku wa Jumatano, ambapo taarifa za kuwasili kwa mwili wa Ngwair zilienea.

Makaburini nako kulikuwa hakutoshi baada ya watu wengi kufurika, huku kila mmoja akiwa na lake, wakiwapo wale waliokwenda kwa ajili ya kuangalia wasanii wao.

HII INASHANGAZA LAKINI NI KWELI: ATEMBEA NA NYUMBA YAKE KWA MIAKA 5 AKIIBEBA. MCHEKI HAPA

clip_image001Anaitwa Liu Lingchao nimchina ambaye amekuwa akitembea kwa  zaidi ya miaka mitano sasa akiibeba nyumba yake mabegani na kuzunguka nayo kutoka sehemu moja kwenda nyingine.


 

HUYU HAPA NDIO KADA WA CHADEMA ALIMWA SHOKA LA MGONGONI MAPEMA HII LEO

Mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni kada wa CHADEMA amelimwa shoka la mgongoni na watu wanaodaiwa kuwa ni walinzi wa CCM wakati wa harakati za kampeni za uchaguzi wa udiwani huko Arusha..

Mtu huyo aliyefahamika kwa jina moja la Amos amelazwa katika hospitali ya Mount Metu mkoani humo...

Mtandao huu unaendelea kufuatilia chanzo halisi na undani wa tukio hilo 
 
KWA HISANI YA  shiladeux.blogspot.com

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA MOROGORO MAZISHI YA MANGWEA


Jeneza lenye mwili wa Albert Mangweha likishushwa kaburini.
M2 THE P amefanikiwa kutoa salamu zake za mwisho kwa rafiki yake kipenzi ambaye alikuwa naye huko Afrika kusini tena walikuwa ndani ya chumba kimoja kabla ya mauti kumkuta Ngwea.
Rafiki wa karibu wa marehemu Albert Mangweha, Mgaza Pembe 'M 2 The P' akiumuaga swahiba wake katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. 

PICHA KWA HISANI YA MITANDAO MBALIMBALI