Na Freddy Macha.
BABU wa fasihi ya Kiswahili, Shaaban Robert alifariki mwezi huu mwaka 1962. Ingetakiwa sikukuu ya kifo chake yaani Juni 20 ifanyiwe maadhimisho kila mwaka. Sisi na wenzangu wa Bendi ya Sayari tuliwahi kusheherekea kwa maonyesho ya 1983. Hazina hii tukufu ya taifa inatakiwa zaidi ya hilo.

Moja ya vitabu vyake babu ni “Kielezo cha Fasili”
kilitolewa upya na mwongozi wa wachapishaji Tanzania; “Mkuki na Nyota”
,2004 na kinafafanua mashairi yake kwa wasomaji mintaarafu ya kujenga
mapafu kilugha.
Ananyambua Shairi la “Jina”: “Mwanadamu mwenye
fikra njema huacha fahari au sifa kwa wat
u ambayo vizazi vyake vya nyuma yake hupenda kuiona na ambayo itakuwa kama hazina kwa watu wote katika dunia.”
u ambayo vizazi vyake vya nyuma yake hupenda kuiona na ambayo itakuwa kama hazina kwa watu wote katika dunia.”
Albert Mangwea hakuwa Shaaban Robert; amefariki
akiwa na miaka 31 tu. Lakini Mangwea au Mangair alitumia fani ya ushairi
kuchangia kuiendeleza fasihi ya Kiswahili na kipaji chake alichomegewa
na Muumba.
Kifo hiki kilichokua Usauzi (Afrika Kusini)
kimezungumziwa na kinaendelea kuzungumziwa. Mwaka jana wakati kama huu,
Tanzania ilimpoteza Steve Kanumba. Vifo vya chipukizi hawa vimeacha
utata na mijadala marefu.
Mangwea alifia ughaibuni.
Maisha ugenini ni magumu maana habari huwa hazitangazwi sana. Mbali na taratibu za kisheria, kinachongojewa kutufariji huwa viongozi wa dini na Serikali.
Maisha ugenini ni magumu maana habari huwa hazitangazwi sana. Mbali na taratibu za kisheria, kinachongojewa kutufariji huwa viongozi wa dini na Serikali.
Vipo vifo vya aina nyingi. Ila vifo vinapokuwa na
utata husubiri mkono wa sheria utubembeleze. Kanumba alifuatiliwa na
mashtaka ya msichana aliyekuwa naye; Mangwea, hatuyajui bado
kiuhakika...
Miaka iliyopita habari za vifo vya Waafrika hasa
zile zilizohusiana na Ukimwi au dawa za kulevya hazikuwekwa wazi, sababu
ya aibu, miiko na staha. Nakumbuka wanamuziki wawili maarufu Hukwe
Zawose na mpwa wake, Charles Zawose walipofariki, wanahabari hatukueleza
chanzo ili kuheshimu hisia za familia zao.
Magazeti ya ughaibuni, walakini, hayakupepesa.
Mwanamuziki Charles Zawose alifariki ghafla
akijitayarisha kupanda ndege Sweden alikokuwa akifanya maonyesho ya
muziki wa kijadi, 2004. Kwa kuwa Charles na baba yake mkubwa
walishajenga majina ugenini habari zilichambuliwa katika magazeti
viongozi. Mwandishi John Lusk wa “Independent” gazeti linaloheshimika
sana Uingereza aliandika:
“Kifo kimenyamazisha moja ya himaya kubwa ya
familia ya wanamuziki wa Tanzania... Walikuwa mabalozi viongozi wa
muziki wa Kigogo.” Akaongeza kuwa Zawose amefariki kutokana na “maradhi
yaliyosababishwa na Ukimwi.”
Nyumbani, lakini, ugonjwa haukutajwa.
CHANZO MWANANCHI.
CHANZO MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment