Hapa
jeneza la Ngwair linaingizwa karubini, ikiwa ni picha inayoonyesha kuwa
hatutaweza tena kukutana na msanii huyu hapa chini ya jua. R.I.P
Ngwair.....MAELFU
ya watu walijazana leo katika Mkoa huu wa Morogoro kwa ajili ya mazishi
ya msanii Albert Mangweha Ngwair, huku aliyepata naye matatizo nchini
Afrika Kusini, Mgaza Pembe M to The P naye akiwa miongoni mwa
waliohudhuria mazishi ya Ngwair.
Hapa
M to The P akilia baada ya kupita kwenye jeneza la Ngwair katika Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika Kihonda
Kanisani jioni yake.
Mama wa Ngwair akizungumza na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Joel Bendera, leo mjini Morogoro, kabla ya mazishi ya msanii huyo wa Hip Hop Tanzania |
Mwili wa Ngwair unaingizwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Hapa
watu wanakanyagana kwa ajili ya kujipanga mstari kwenda kumuaga
marehemu Ngwair, leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro ulikuwa umejaa watu, sambamba na wale
waliojipanga barabarani kwa ajili ya kuangalia msafara wa Ngwair
uliofunika mji wote siku ya leo.
Tukio
la kuzikwa lilitanguliwa na shughuli ya uagaji iliyofanyika pia katika
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, baada ya kuona mkanyagano wa watu
wengi nyumbani, usiku wa Jumatano, ambapo taarifa za kuwasili kwa mwili
wa Ngwair zilienea.
Makaburini
nako kulikuwa hakutoshi baada ya watu wengi kufurika, huku kila mmoja
akiwa na lake, wakiwapo wale waliokwenda kwa ajili ya kuangalia wasanii
wao.
0 comments:
Post a Comment