Blogger Widgets

Sunday, November 3, 2013

ARUSHA YAONGOZA KWA BANGI


Na Mwandishi Wetu, Ausha
IMEBAINIKA kuwa Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kilimo haramu cha bangi ambayo imekuwa ikiharibu vijana wengi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
Akizungumzia ishu hiyo wakati wa uteketezaji wa mashamba ya bangi wilayani Arumeru jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alikemea vikali juu ya ustawishaji wa mmea huo huku akisisitiza kula sahani moja na wahusika.
Kamanda huyo aliwataka raia wema kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mara moja wanapogundua uhalifu wa aina hiyo na mwingine wowote.

0 comments:

Post a Comment