Blogger Widgets

Thursday, November 14, 2013

Wafahamu watanzania wanne walioingia kwenye orodha ya matajiri 50 wa Afrika-2013

 Rostam Aziz aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, Said Bakhresa na mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji wameingia kwenye orodha ya Forbes ya watu 50 matajiri zaidi barani Afrika.

Rostam Aziz ndiye aliyeibuka kidedea kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 1 na kukamata nafasi ya 27 kwenye orodha hiyo.

Huku Mwenyekiti na mtendaji wa makampuni IPP,Reginald Mengi ameshika nafasi ya 34 akiwa na utajiri wa dola Milioni 550  kwenye orodha hiyo ya Forbes.

Kwenye nafasi ya 38 ya orodha hiyo, imeshangaza kuona Said Salim Bakhresa na Mohamed Dewji wakiwa sawa kwa utajiri wa dola milioni 500 kila mmoja.

0 comments:

Post a Comment