Blogger Widgets

Friday, September 14, 2012

USAILI WA MAISHA PLUS 2012 UNAENDELEA MIKOANI

                          Hii ndiyo team nzima ya maisha plus inayofanya usaili mikoani kote Tanzania.

                                                Dada mwanahamisi akiongeoa na vijana

Baada ya kukamilisha usaili Dodoma, Kahama, Kagera,Singida, Mwanza, Morogoro, Iringa sasa usaili unaelekea mkoani Mbeya ambapo utafanyika Sept 15.
Crew nzima ya Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula inayodhaminiwa na banki ya NMB na Oxfam  baada ya hapo itaendelea na safari kutoka Mbeya moja kwa moja mpaka Kilwa, ambapo itafanya usaili  Septemba 17, kesho yake siku ya Septemba 18 usaili utaelekea Masasi  mkoani Mtwara.Septemba 20 sasa itakuwa ni zamu ya wakazi wa Zanzibar baada ya kumpata mwakilishi wa zanzibar sasa hapo ndipo team nzima ya maisha plus itarejea Dar es Salaam kwa ajili ya usaili ambao utakao fanyika tarehe 22 na 23
Kitakachofuatia baada ya usaili wa Dar.Kipindi hiki cha Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula  kitaanza rasmi  kuonekana katika runinga yako.Usikae mbali na TBC1 kwasababu ndiyo itakayokusafirisha nchi nzima ukiwa kwenye sofa lako nyumbani.

0 comments:

Post a Comment