Blogger Widgets

Friday, December 21, 2012

MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAMPA DHAMANA LULU

http://www.facebook.com/TAJOA
Msanii Lulu kula Xmas akiwa kwao
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam asubuhi ya leo imempa dhamana msanii Elizabeth Michael baada ya kupitia vifungu kadhaa na kuona kesi yake ya kuua bila kukusudia inadhaminika.

Kwa maana hiyo, Lulu sasa atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya wa 2013 akiwa na familia yake, ndugu, jamaa na marafiki.

Msanii huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusidia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam asubuhi ya leo imempa dhamana msanii Elizabeth Michael baada ya kupitia vifungu kadhaa vya sheria na kuona kesi yake ya kuua bila kukusudia anauwezo wakupata dhamana

Kwa maana hiyo, Lulu sasa yuko na familia yake vilevile atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya wa 2013 akiwa na ndugu, jamaa na marafiki.

Msanii huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusidia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru. Endelea kutembelea theHOODinfotainment itakuleta muendelezo wa stori hii mwanzo hadi mwisho.

0 comments:

Post a Comment