Posted: 1st September 2012 by Yusha.
Katika gazeti kubwa la burudani
Tanzania la Baabkubwa lililotoka hivi karibuni ambalo husomwa na
wabongo wengi wanaopenda stori za burudani kiliandikwa kichwa cha habari
kwamba Marlaw ameshindwa kabisa kumpa mimba mkewe Besta ambae ni msanii
pia.
Kutokana na hilo Marlaw aliomba namba kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM ili kukanusha hizo taarifa.
Namkariri akisema “swala la
mimi kumpatia mimba mke wangu au uzao wa familia yangu ni swala langu
binafsi, sidhani kama ni swala la Baabkubwa, mi sijapenda alafu na
dizaini walivyoelezea yani ile interview mimi ninavyozungumza yale sio
maneno yangu”
Kwenye line nyingine
amesisitiza kwamba “kama walinipigia simu basi ningependa kama
wangeandika kile hasa ambacho hasa mimi nimekisema, nakumbuka
walishawahi kunipigia simu lakini tukazungumza lakini mazungumzo hayakua
vile jinsi ilivyokuja kuandikwa, yamebadilishwa”
“sitochukua hatua yoyote nataka
tu wanipigie simu waniambie samahani, mtu ataenipigia simu anipigie tu
tumalize tuongee tu yaishe, kama wangependa kuandika kwenye gazeti
lijalo waandike kile nilikiongea”
Baada ya hayo nilipochek na Baabkubwa walikua kwenye kikao lakini wakasema time ikifika msemaji atazungumza.
0 comments:
Post a Comment