Posted: 8th September 2012 by yusha shabani
Zaidi ya waumini mia tatu wa
dini ya kiislam jana september 7 waliandamana mpaka Wizara ya mambo ya
ndani wakishinikiza jeshi la polisi kuwaachia baadhi ya viongozi wa
kiislam waliokamatwa kwa kupinga zoezi la sensa.
Waumini hao walifika kwenye
makao makuu wakitaka kuonana na waziri wa mambo ya ndani ili asikilize
madai yao ambapo walifanikiwa kuonana nae na baada ya mazungumzo marefu
kati ya serikali na waumini hao, serikali imekubali kuwaachia huru
Waislamu wote waliokamatwa kupinga zoezi la sensa ya watu na makazi.
Mwandishi wa habari Masoud
ambae alikuepo kwenye eneo la tukio aliripoti na namkariri akisema
“ujumbe uliokwenda kuonana na viongozi wa Wizara ya mambo ya ndani
umekubaliana kwamba wale waislam wote nchi nzima Bara na visiwani ambao
walikua wameshikiliwa kutokana na kupinga sensa, wataachiwa huru na
maandamano kuisha na hali imekua shwari, serikali imekubali kuwaachia
huru”
0 comments:
Post a Comment