Kuna
sababu kubwa kwanini Bongo5 haikuandika habari iliyodai kuwa Nay wa
Mitego na Chidi Benz wamepatanishwa na Cassim Mganga na sasa ni amani
tu. Kilichotokea sasa ni kwamba, Chidi Benz anamuita Cassim Mganga
Mchawi, kauli ambayo ambayo iliwafanya hivi karibuni watukanane matusi
ya nguoni Club Billicanas, na kama wasingekuwepo watu waliowazuia,
wangetoana meno siku hiyo.

“Mwacheni asinizingue mimi, nakosea mimi kila siku,” anasikikia
Cassim akiongea kwenye audio iliyorekodiwa na kuifikia mikono ya Soudy
Brown wa U Heard. “Mimi nimekosea nini Benz apige was**ge wengine mimi
hawezi kunifanya lolote, msimshike, aniguse halafu aone. Mimi si maisha
yangu, nahangaika nafanya muziki wangu wanasema mimi mchawi, mimi nina
familia yangu, mimi sio mchawi, namroga nini mimi, yeye stress zake,
anavuta unga, mimi namsingizia? Kila mtu anajua, yeye si life yake
amechagua? Asinizingue, mimi mwanaume power kama yeye.”
Sikiliza mwenyewe hapa.







0 comments:
Post a Comment