Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Friday, August 31, 2012

HII NI MAALUM KWA MASHABIKI WA CHELSEA TU.

Posted: 31st August 2012 by Yusha 
Hizi ni picha za wachezaji wa Chelsea wakiwa mazoezini kujiandaa na mechi yao ya leo na Atletico Madrid kwenye UEFA Super Cup, timu ambayo Fernando Torres aliwahi kuichezea kabla ya kujiunga na Liverpool 2007 na anasema ndio club pekee anayoizimia sana duniani.
.
.
Kipa Petr Cech.
.
.

'Campus Divas For Rich Men’ kundi la Facebook wanapouzwa wanachuo wa Kenya


Jane 18 has just finished high school and will be joining UoN she wants a rich dude who is willing to pay her half % school fees

“Sisi madiva tuna gharama, NYWELE, zinataka dawa! MASIKIO yanataka,hereni!! MACHO yanataka wanja na shadow! PUA inatka kipini! MDOMO, unatka lipstic! USO unataka poda na foundation! SHINGO inataka cheni! MATITI yanataka sidiria! MIKONO inataka Bangali! VIDOLE vinataka, Pete! KIUNO kinataka shanga. MA***KO yanataka chupi MIGUU inataka hina rangi na viatu. KAMA HUNA MKWANJA POLEEEEEEE,” ni baadhi ya status zinazosomeka kwenye ukurasa uitwao 'Campus Divas For Rich Men’.

Ni ukurasa maarufu sana kwenye Facebook sasa hivi nchini Kenya, ukiwa na likes 34,339. 

Ukurasa huu huonesha picha za wasichana ‘wanaodaiwa kuwa ni wanachuo’ wakijiuza na kutafuta wanaume wenye fedha ili wawatimizie haja zao.
Hata hivyo kwa uchunguzi uliofanywa na gazeti la Daily Post, umegundua mtu aliyeufungua ukurasa huo ambao kiukweli picha na majina anayoyaweka sio vya kweli.
Huyu ndiye aliyeanzisha ukurasa huo

Mtu huyo ni mvulana ambaye inasemekana kuwa alikuwa akimpenda msichana aitwaye Samira Osman lakini alipokataliwa, aliamua kufungua ukurasa huo kwa hasira.
Mkononi amejichora jina la Samira, msichana aliyemkataa
Hivi ndivyo anavyoweka picha za wasichana zikiwa na maelezo kuwa wanataka wanaume matajiri huku maelezo akiyaandika mwenyewe.
Candy 20 Kenyatta university wants a rich man who can cater for her needs

MWANAUME NA MWANAMKE WAFUPI DUNIANI WAKUTANA




Kwa mara ya kwanza katika historia, Mwanaume mfupi na mwanamke mfupi duniani wamekutana, Mwanaume mfupi anayeitwa Chandra Bahadur Dangi mwenye miaka 72 anatokea Nepal anaurefu wa inchi 21.5 na Mwanamke mwenye miaka 18 Jyoti Amge anatokea Nagpur India anaurefu wa ichi 25.
Ilikuwa ni katika kupiga picha kwa ajili ya promo ya maandalizi ya kitabu cha Guiness World Records kitakachotoka Septemba 2013.

Tuesday, August 28, 2012

HIVI UMESIKIA ALICHOSEMA T.I.D KUHUSU TAARIFA ZA KUTAKA KUMUUA ALLY KIBA? HII NDIO STORI YENYEWE.

Posted: 29th August 2012 by yusha
Ally Kiba na T.I.D

Kwenye U heard ya XXL Clouds Fm august 28 2012 Gossip Cop Soudy Brown ameripoti kwamba kuna mwanamke aliekamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa saa nane wakati akiwa kwenye mipango ya kumuua msanii wa bongo fleva Ally kiba.
Baada ya kuhojiwa na polisi kwa saa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.
Alipohojiwa na Soudy Brown, T.I.D amesema “kwa nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani? toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi,nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe”
Soudy alipomtafuta meneja wa Ally Kiba alijibiwa “hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari sasa hivi  lakini ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua”

Monday, August 27, 2012

JINSI MASHEHE WALIVYOKWEPA KUHESABIWA KWENYE SENSA.

Posted: 28th August 2012 by yusha

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ramadhani Maneno wa pili kutoka kulia.
Zoezi la sensa ya watu na makazi kwenye mkoa wa Kigoma lilipata ugumu kutokana na waumini wa dini ya kiislamu wanaopinga kuhesabiwa kukimbilia misikitini hivyo kutofikiwa na makarani waandikishaji.
Mkuu wa wilaya Kigoma Ramadhani Maneno amesema kwenye pitapita yao kufanya tathmini wamekutana na ugumu huo na tayari wameanza kuufanyia kazi, maeneo ambayo wamegundua tatizo hilo ni pamoja na Mwandiga na Katonga ambapo licha ya kutaka kuongea na viongozi wa misikiti hiyo, wameshindwa kupata ushirikiano wowote hivyo  amesema kamati ya ulinzi na usalama inatarajia kukaa kujadili ili kuona hatua za kuchukua.

hii ni moja ya baadhi ya picha zilizosambaa za waumini wa dini ya kiislamu kupinga ishu ya sensa.
Amekaririwa akisema “kuna baadhi ya viongozi wa kiislam wameshawishi waislam wenzao kwenda kulala misikitini ili kusiwe na nafasi tena kwa makarani wa sensa kuingia misikitini, nilipojaribu kwenda kwenye msikiti wa Mwandiga kujaribu kushawishi niongee na viongozi wao, sikufanikiwa”
Mwandishi Fadhili Abdallah anasema Mkuu huyo wa wilaya amethibitisha jumla ya kaya 40 kati ya 64 kwenye kijiji cha Bubango kata ya Bitale Kigoma Vijijini, zimekataa kuandikishwa kufuatia maelekezo ya viongozi wa kaya hizo.

HIVI NDIVYO SERENGETI FIESTA 2012 TANGA ILIVYOKUA.

Posted: 28th August 2012 by yusha
.
B12 mkali wa XXL ya CLOUDS FM ndio alihost show akishirikiana na Adam Mchomvu.
Adam Mchomvu, mkali mwingine wa XXL aliehost show fresshhhh kabisa.
Nuru akiwa kazini.
.
.
.
Recho nae alifanya poa sana.. kuna video yake hapo chini jinsi alivyovionyesha viuno pamoja na dancers wake.
.
.
Stamina kama kawa.
Dancers wa THT, ukali wao unaweza kuuona kwenye video yao hapo chini pia..
Shetta.
Dancers wa Shetta.
Ferooz.
Baadhi ya wakali wa bongo movie walikuepo pia… hapa ni Steve Nyerere akiwa na Shilole.
.
Steve Nyerere na Aunt Ezekiel.
.
Wema Sepetu, Aun Ezekiel, Shilole na JB.
CMB Prezzo.
.
.
.
.
Linah Sanga.
.
endelea kutembele http:yushathhood.blogspot.com itakua inakuletea matukio yote ya SERENGETI FIESTA 2012 na retiba nzima ya show zote zitakazofanyika katika kila mkoa.

MSIMAMO MPYA WA SAMUEL ETOO KUHUSU TIMU YAKE YA TAIFA.

Posted: 28th August 2012 by yusha 
Mwandishi Shaffih Dauda wa shaffihdaud.com ameripoti kwamba mchezaji Samuel Eto’o  amekataa kuichezea Cameroon katika kutekeleza mgomo wake dhidi ya kile alichokiita mpangilio mbovu na mazingira yasioeleweka katika kikosi cha timu ya taifa.
Etoo alikuwa kwenye kikosi cha Cameroon kwa ajili ya kupambana na Carpe Verde katika michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika September baada ya kumaliza adhabu yake kufungiwa miezi nane.
Lakini Eto’o alisema kwenye barua yake aliyoiandika kwa shirikisho la soka la Cameroon kwamba hatoweza kurejea kwenye timu ya taifa kwa sababu matatizo yote yaliyomfanya akafungiwa bado hajatafutiwa ufumbuzi.
Eto’o ambaye ameshaichezea nchi yake mechi 109 na kufunga magoli 54, alifungiwa kutokana na kuongoza mgomo wa wachezaji baada ya kutolipwa posho zao, shirikisho la soka la Cameroon liliamuarifu Eto’o na mwanasheria wake pamoja na timu yake ya Anzhi Makhachkala kwamba kifungo chake kimeisha mapema wiki hii ambapo baada ya hapo kocha Denis Lavagne akamchagua Eto’o katika kikosi chake cha wachezaji  23 kwa ajili ya kucheza dhidi ya Cape Verde tarehe 8 mwezi ujao kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya kufuzu kushiriki AFCON 2013.
Lakini nahodha wa Cameroon bado amekosa furaha dhidi ya masuala ya uongozi mbovu kwenye timu ya taifa na suala lao la kuwapandisha wachezaji ndege daraja la pili tena kwenye safari ndefu – na kutokana na sababu hizo mshambuliaji huyo wa zamani wa Barca amejiondoa kwenye timu ya taifa.
Amekaririwa akisema “timu yetu ya taifa inaendelea kupotea kutokana na mazingira mabovu na mpangilio usioleweka, vitu ambavyo haviendi sawa na michezo ya kisasa, nina mashaka mashabiki wa timu ya taifa wataelewa hatua yangu hii ambayo mlengo wake mkuu ni kubadilisha mambo yote ya ovyo, timu ni taasisi yenye heshima ambayo imechangia sana mafanikio ya nchi”

Nape Aikomalia Chadema, Akataa Kuomba Radhi




Akataa kuomba radhi, asema tuhuma atazithibitisha mahakamani, Amtaka Dk. Slaa kuandaa bilioni 3 na shilingi moja. Ni kwa kudai CCM inaingiza silaha nchini.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amewataka Chadema kwenda mahakamani haraka badala ya kusubiri kuombwa radhi kama walivyotaka ili kusafishwa dhidi ya madai ya chama chao kupewa mabilioni ya fedha na mataifa tajiri.

Aidha amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa kuiomba radhi CCM la sivyo itamburuza mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3 na shilingi moja, kwa kuituhumu uongo kwamba imeingiza silaha kutoka nje ya nchi tena bila kulipia ushuru.

Nape alisema hayo leo Agosti 27, 2012, kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam.

"Bila shaka mmesikia jana Chadema wakinitaka niombe radhi au wananipeleka mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3, kwa madai eti nimesema Chama hicho kinapata mabilioni ya fedha kutoka kwa mataifa tajiri. Mkubwa hatishiwi nyau, nawataka waende haraka mahakamani wala wasisubiri hizo siku saba", alisema Nape.

Alisema, CCM inao ushahidi wa kutosha kuhusu madai aliyotoa Nape dhidi ya Chadema na kwamba huyo tayari kutoa uthibitisho huo mahakamani badala ya kuomba radhi.

"Nadhani wakienda mahakani itapendeza zaidi maana huko ndiko pazuri kutoa uthibitisho kuhusu tuliyosema, na ninawahakikishieni tukishathibitisha na Msajili wa Vyama akaupata uthibitisho huo chama chao kinafutwa", alisema.

Kuhusu CCM kumburuza Dk. Slaa mahakamani, Nape alisema, ameshawaagiza wanasheria wa Chama, kuandaa barua ya kusudio la mashitaka hayo, na Dk. Slaa atapelekewa ili aamue kama ataomba radhi au atakuwa tayari kwenda mahakamani.

"Wakati wanakwenda mahakamani, Chadema wamwambie babu yao ajiandae kuomba radhi au kuburuzwa mahakamani kuilipa CCM fidia ya sh. bilioni 3 na shilingi moja kwa kuizushia CCM uongo kwamba inaingiza silaha nchini tena", alisema Nape.

Bashir Nkoromo
Blogger & Senior Photojournalist
Uhuru Publications Ltd,
Publishers of Uhuru, Mzalendo and Burudani tabloids
Cell; +255 712 498008, +255 789 498008, +255 773 600007 +255 756 646131
E-mail: nkoromo@gmail.com, bnkoromo@yahoo.com.
P O Box 9221, Dar es Salaam.Tanzania, East Africa

Sunday, August 26, 2012

CLINIC YA BASKETBALL YA HASHEEM THABIT NA LUOL DENG





Saturday, August 25, 2012

SHERIA MPYA YA VYOO VYA UMMA CHINA: NZI WASIZIDI WAWILI



Sheria hiyo inakataza choo kuwa na zaidi ya nzi wawili kwa wakati mmoja.Sheria hiyo iliyowekwa na halmashauri ya mannispaa ya jiji la Beijing inalenga kuhakikisha hali ya usafi katika vyoo vinavyotumiwa na jamii.
Hata hivyo haijawekwa wazi ni hatua gani zitachukuliwa iwapo nzi wa watu atakutwa chooni.
Sheria nyingine ni kuhakikisha vyoo vinasafishwa kila mara na matumizi ya vifaa vyakisasa na mafunzo ya kutosha kwa watu wanaovitazama vyoo hivyo.
Mwandishi wa BBC mjini Beijing amesema sheria hizi mpya ni mahsusi kusaidia watu wengi mjini humo ambao hawana vyoo majumbani mwao na wanategemea vyoo vya umma. Bila shaka watakuwa wakitazama huko na huko kutafuta nzi wa tatu yuko wapi..