Mmoja
wa majeruhi wa ajali ya Fuso iliyotokea Wilayani Nkansi jana Mkoani
Rukwa akiwa amelazwa katika Hospitali kuu ya Mkoa wa huo huku akiendelea
kupatiwa matibabu. Watu saba walifariki papo hapo katika ajali hiyo
iliyohusisha Fuso iliyokuwa imebeba mizigo na abiria ambapo majeruhi
walikuwa 37, Mpaka sasa jumla ya abiria waliofariki ni 10 na wengine
bado wapo hospitalini hapo wakiendelea kupata matibabu na wengine
walisharuhusiwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimpa pole mmoja wa majeruhi
walionusurika kwenye ajali hiyo mbaya kati ya ajali zilizowahi kutokea
Mkoani Rukwa. Mkuu huyo wa Mkoa alisikitishwa na ajali hiyo iliyomfanya
apige marufuku usafiri unaohusisha mizigo na abiria kwa wakati mmoja.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Emanuel Mtika akitoa
maelezo ya majeruhi kwa Mkuu wa Mkoa huo alipotembelea kuwaona kufuatia
ajali mbaya iliyotokea jana na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine
zaidi ya 30 kujeruhiwa.
Agnes
ni mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali hiyo akiwa na watoto
wake wawili wadogo wanaonekana pichani na mumewe ambaye alisharuhusiwa
baada ya kupata nafuu.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Balozi wa Kenya
nchini Tanzania Balozi Mutinda Mutiso ofsini kwake leo alipotembelewa
na balozi huyo ambaye yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi yenye lengo
la kudumisha uhusiano kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kuangalia
fursa za uwekezaji zinazopatikana katika Mikoa ya nyanda za juu kusini.
Balozi huyo anategemea kwenda Mkoa jirani wa Katavi ambapo pamoja na
shughuli nyingine ataembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi. Mkuu huyo wa
Mkoa wa Rukwa amemuhakikishia balozi huyo uwepo wa fursa nyingi za
uwekezaji Mkoani Rukwa ikiwemo Kilimo, Utalii, Uvuvi, Elimu na Biashara.
Alimueleza kuwa kazi kubwa inayoendelea hivi sasa ni utengaji maeneo
maalum ya uwekezaji.
Mazungumzo yakiendelea ofsini kwa Mkuu wa Mkoa.
Balozi
wa Kenya nchini Tanzania Mutinda Mutiso akielezea lengo la ujio wake
Mkoani Rukwa mbele ya Mkuu wa Mkoa huo na viongozi wengine wa Serikali
ya Mkoa mapema leo ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huo. Aliiomba pia Serikali
ya Tanzania kujenga urafiki na wageni ili kuimarisha mahusiano mazuri
amabayo yamekwishajengeka kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya.
Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimsihi balozi huyo na nchi yake
ya Kenya kusaidiana na Tanzania kudumisha amani iliyopo ili Afrika ya
Mashariki pawe pahala salama pa kuishi na kufanya maendeleo ikiwemo
uwekezaji ambao hauwezi kustawi pasipokuwa na amani.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima hapo kabla
akimtambulisha balozi wa Kenya kwa viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa
Ofsini kwake alipoenda kumsalimia kabla ya kuonana na Mkuu wa Mkoa huo.
Kutoka
kulia ni Afisa Mkuu wa Jeshi la Usalama Barabarani Mkoani Rukwa, Katibu
Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Samson Mashalla, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Rukwa (RPC) Jakob Maruanda na Katibu Tawala Msaidizi
Miundombinu Francis Kilawe wakiwa kwenye meza ya mazungumzo na Balozi
huyo wa Kenya.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa agizo kwa Kamanda wa
Polisi Mkoa huo Jakob Maruanda mbele ya waandishi wa habari na viongozi
wengine wa Mkoa huo akiwemo Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed
Chima, agizo ambalo limepiga marufuku usafirishaji wa abiria katika
magari ya mizigo. Alimueleza kuwa yeyote atakayekutwa akisafirisha
abiria kwenye malori ya mizigo achukuliwe hatua kali za kisheria
kudhibiti ajali za namna hiyo kutokea.Picha na Habari zote na Hamza Temba-Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
0 comments:
Post a Comment