Kamanda
wa Polisi mkoa wa (ACP) Liberatus sabas akiwaonyesha waaandishi wa
habari silaha aina ya Rifle 458 iliyokuwa inatumiwa na jambazi ambaye
alifariki dunia baada ya kupigwa risasi na askari wa Polisi walipokuwa
wanarushiana risasi katika eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru tarehe
13/08/2012 (Picha na Rashid nchimbi wa Polisi Arusha)
MNAMO
TAREHE 13/08/2012 MUDA WA SAA 8:30 USIKU KATIKA KIJIJI CHA LEVOROSI
KATA YA KIMNYAKI WILAYANI ARUMERU, MTU ASIYEFAHAMIKA JINA, MWANAUME
ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA 28 NA 30 AMBAYE ANADHANIWA KUWA
NI JAMBAZI ALIFARIKI DUNIA AKIWA NJIANI ANAPELEKWA HOSPITALI KWA AJILI
YA MATIBABU BAADA YA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI MARA BAADA YA
KUKAHIDI AMRI HALALI YA KUJISALIMISHA.
TUKIO
HILO LILITOKEA WAKATI ASKARI WA JESHI LA POLISI NA JAMBAZI HUYO AMBAYE
KWA SASA NI MAREHEMU WAKIJIBIZANA KWA KURUSHIANA RISASI NA HIVYO ASKARI
KUFANIKIWA KUMPIGA RISASI TUMBONI NA MARA BAADA YA UPEKUZI WALIFANIKIWA
KUMKUTA AKIWA NA BUNDUKI AINA YA RIFLE 458 YENYE NAMBA 7052602464 MODEL
ZKK-620 AMBAYE ILIKUWA IMEKATWA MTUTU PAMOJA NA KITAKO IKIWA NA RISASI
MBILI.
AWALI
ASKARI HAO WALIKWENDA KATIKA NYUMBA YA MAREHEMU NA KUIZINGIRA NA
MAREHEMU ALISHTUKA BAADA YA KUSIKIA MILIO YA MBWA NA AKAFUNGUA MLANGO
NA MARA ALIPOGUNDUA KUNA ASKARI ALIANZA KUWARUSHIA RISASI MBILI ILI
APATE NJIA YA KUTOROKA JAPOKUWA ALIPEWA AMRI HALALI YA KUJISALIMISHA
LAKINI ALIKAIDI.
UCHUNGUZI
WA JESHI LA POLISI ULIBAINI KWAMBA MAREHEMU ALIKUWA ANASHIRIKIANA NA
WENZAKE KATIKA MATUKIO MBALIMBALI YA UHALIFU NA JITIHADA ZA JESHI LA
POLISI ZILIFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WATATU AMBAO WALIKUWA
WANASHIRIKIANA NA MAREHEMU KATIKA MATUKIO YA UHALIFU YALIYOFANYIKA
KATIKA MAENEO TOFAUTI YA NCHI.
WATUHUMIWA
HAO WALIKIRI KUSHIRIKIANA NA MAREHEMU KATIKA MATUKIO MBALIMBALI NA
KUELEZA ANAPOISHI, NDIPO ASKARI WALIPOENDELEA NA UPELELEZI NA SIKU HIYO
YA TAREHE 13/08/2012 WALIFANIKIWA KUIZINGIRA NYUMBA HIYO AMBAPO
KULITOKEA MAJIBIZANO YA RISASI NA HATIMAYE MTUHUMIWA KUPIGWA RISASI YA
TUMBO NA KUFARIKI DUNIA AKIWA ANAPELEKWA HOSPITALI KWA AJILI YA
MATIBABU.
MARA
BAADA YA KUIPATA BUNDUKI HIYO KUTOKA KWA MAREHEMU KATIKA UCHUNGUZI WETU
TULIGUNDUA KWAMBA, BUNDUKI ILIYOKUWA INATUMIWA NA MAREHEMU PAMOJA NA
WENZAKE ILIPORWA TOKA KWA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GABRIEL S/O
WILLIAM MKAZI WA SEKEI SIKU YA TAREHE 01/04/2012 MUDA WA SAA 4:00 USIKU
AMBAPO MMILIKI HUYO ALIVAMIWA NA MAJAMBAZI HAO AKIWA ANAINGIA KATIKA
GETI LA NYUMBA YAKE HUKU AKIWA NA GARI YAKE AINA YA SUZUKI ESCUDO YENYE
NAMBA ZA USAJILI T. 887 APC.
KATIKA
TUKIO JINGINE LILITOKEA HUKO ILBORU TAREHE 02/08/2012 USIKU ASKARI WA
JESHI LA POLISI MKOANI HAPA WAKIWA DORIA WALIFANIKIWA KUKAMATA BUNDUKI
MOJA AINA YA SHORT GUN-GREENERS GP GUN IKIWA IMEFUTWA NAMBA BAADA YA
WATU WANAOAMINIKA KUWA NI MAJAMBAZI KUITELEKEZA BAADA YA KUGUNDUA KUWA
WANAFUATILIWA NA ASKARI.
TUKIO
HILO LILITOKEA BAADA YA ASKARI HAO KULITILIA SHAKA KUNDI LA WATU HAO
NA MARA BAADA YA KUNDI HILO KUGUNDUA KWAMBA NI ASKARI POLISI WALIANZA
KUKIMBIA NA MMOJA WAO KUTUPA CHINI MFUKO MWEUSI NA MARA BAADA YA ASKARI
KUUPEKUWA WALIONA BEGI DOGO AMBAPO NDANI YAKE WALIIKUTA BUNDUKI HIYO
AMBAYO ILIKUWA IMEKATWA MTUTU NA KITAKO IKIWA NA RISASI 12.
MPAKA
HIVI SASA WATUHUMIWA HAO BADO HAWAJAPATIKANA NA JESHI LA POLISI
LINAENDELEA NA JUHUDI ZA KUWATAFUTA. MAFANIKIO HAYO YAMETOKANA NA MSAKO
ENDELEVU ULIOANZA TOKA TAREHE 08/06/ MWAKA HUU KATIKA MAENEO MBALIMBALI
YA MKOA HUU. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) LIBERATUS SABAS
0 comments:
Post a Comment