Posted: 17th August 2012 by yusha shabani
Kwanza poleni sana katika
kipindi hiki kigumu cha kuchukuliwa mkali Robin van Persie ambae
ameingia kwenye familia ya Alex Ferguson.
Ninachotaka kuwaambia ni ripoti
ya gazeti la The Sun Uingereza kuandika kwamba kocha Arsene Wenger wa
Arsenal amesisitiza kwamba hatonunua striker mwingine ili kuchukua
nafasi ya Robin Van Persie.
Yani kasema washambuliaji
Olivier Giroud na Lukas Podolski wanatosha kabisa kuziba nafasi ya Van
Persie na muda wote wawili hao walikua wakiandaliwa kuchukua hiyo
nafasi.
Kocha huyo Mfaransa mwenye
miaka 62 toka aletwe duniani, amesema japo inauma kupoteza mchezaji kama
Van Persie kulikua hakuna njia yoyote isipokua kumuuza tu.
Kwenye line nyingine ni kwamba
kocha wa Manchester United amesema anaamini jumatatu Van Persie
atacheza kwenye mechi dhidi ya Everton.
August 15 2012 usiku ndio
ilithibitisha kumchukua Van Persie ambapo Fergie alithibitisha kwamba
mkali huyo alitarajiwa kufika Old Traford August 16 jioni kuonana na
madaktari wa club hiyo na ana imani yote yaliyobakia yatamalizika kabla
ya mechi ya jumatatu.
Kwa kumalizia amefananisha
uwepo wa Wyne Rooney, Van Persie, Chicharito na Danny Welbeck kama
ilivyokua 1999 kwa uwepo wa vichwa vikali kama Yorke, Cole, Sheringham
and Solskjaer — the four best strikers in Europe.
0 comments:
Post a Comment