Sheria
hiyo inakataza choo kuwa na zaidi ya nzi wawili kwa wakati mmoja.Sheria
hiyo iliyowekwa na halmashauri ya mannispaa ya jiji la Beijing inalenga
kuhakikisha hali ya usafi katika vyoo vinavyotumiwa na jamii.
Hata hivyo haijawekwa wazi ni hatua gani zitachukuliwa iwapo nzi wa watu atakutwa chooni.
Sheria
nyingine ni kuhakikisha vyoo vinasafishwa kila mara na matumizi ya
vifaa vyakisasa na mafunzo ya kutosha kwa watu wanaovitazama vyoo hivyo.
Mwandishi
wa BBC mjini Beijing amesema sheria hizi mpya ni mahsusi kusaidia watu
wengi mjini humo ambao hawana vyoo majumbani mwao na wanategemea vyoo
vya umma. Bila shaka watakuwa wakitazama huko na huko kutafuta nzi wa
tatu yuko wapi..
0 comments:
Post a Comment