Posted: 28th August 2012 by yusha
Mwandishi Shaffih Dauda wa
shaffihdaud.com ameripoti kwamba mchezaji Samuel Eto’o amekataa
kuichezea Cameroon katika kutekeleza mgomo wake dhidi ya kile
alichokiita mpangilio mbovu na mazingira yasioeleweka katika kikosi cha
timu ya taifa.
Etoo alikuwa kwenye kikosi cha
Cameroon kwa ajili ya kupambana na Carpe Verde katika michuano ya kufuzu
kombe la mataifa ya Afrika September baada ya kumaliza adhabu yake
kufungiwa miezi nane.
Lakini Eto’o alisema kwenye
barua yake aliyoiandika kwa shirikisho la soka la Cameroon kwamba
hatoweza kurejea kwenye timu ya taifa kwa sababu matatizo yote
yaliyomfanya akafungiwa bado hajatafutiwa ufumbuzi.
Eto’o ambaye ameshaichezea nchi
yake mechi 109 na kufunga magoli 54, alifungiwa kutokana na kuongoza
mgomo wa wachezaji baada ya kutolipwa posho zao, shirikisho
la soka la Cameroon liliamuarifu Eto’o na mwanasheria wake pamoja na
timu yake ya Anzhi Makhachkala kwamba kifungo chake kimeisha mapema wiki
hii ambapo baada ya hapo kocha
Denis Lavagne akamchagua Eto’o katika kikosi chake cha wachezaji 23
kwa ajili ya kucheza dhidi ya Cape Verde tarehe 8 mwezi ujao kwenye
mchezo wa raundi ya kwanza ya kufuzu kushiriki AFCON 2013.
Lakini nahodha wa Cameroon bado
amekosa furaha dhidi ya masuala ya uongozi mbovu kwenye timu ya taifa
na suala lao la kuwapandisha wachezaji ndege daraja la pili tena kwenye
safari ndefu – na kutokana na sababu hizo mshambuliaji huyo wa zamani wa
Barca amejiondoa kwenye timu ya taifa.
Amekaririwa akisema “timu yetu
ya taifa inaendelea kupotea kutokana na mazingira mabovu na mpangilio
usioleweka, vitu ambavyo haviendi sawa na michezo ya kisasa, nina mashaka mashabiki wa timu ya taifa wataelewa hatua yangu hii ambayo mlengo wake mkuu ni kubadilisha mambo yote ya ovyo, timu ni taasisi yenye heshima ambayo imechangia sana mafanikio ya nchi”
0 comments:
Post a Comment