Posted: 28th August 2012 by yusha
Zoezi la sensa ya watu na
makazi kwenye mkoa wa Kigoma lilipata ugumu kutokana na waumini wa dini
ya kiislamu wanaopinga kuhesabiwa kukimbilia misikitini hivyo kutofikiwa
na makarani waandikishaji.
Mkuu wa wilaya Kigoma Ramadhani
Maneno amesema kwenye pitapita yao kufanya tathmini wamekutana na ugumu
huo na tayari wameanza kuufanyia kazi, maeneo ambayo wamegundua tatizo
hilo ni pamoja na Mwandiga na Katonga ambapo licha ya kutaka kuongea na
viongozi wa misikiti hiyo, wameshindwa kupata ushirikiano wowote hivyo
amesema kamati ya ulinzi na usalama inatarajia kukaa kujadili ili kuona
hatua za kuchukua.
Amekaririwa akisema “kuna
baadhi ya viongozi wa kiislam wameshawishi waislam wenzao kwenda kulala
misikitini ili kusiwe na nafasi tena kwa makarani wa sensa kuingia
misikitini, nilipojaribu kwenda kwenye msikiti wa Mwandiga kujaribu
kushawishi niongee na viongozi wao, sikufanikiwa”
Mwandishi Fadhili Abdallah
anasema Mkuu huyo wa wilaya amethibitisha jumla ya kaya 40 kati ya 64
kwenye kijiji cha Bubango kata ya Bitale Kigoma Vijijini, zimekataa
kuandikishwa kufuatia maelekezo ya viongozi wa kaya hizo.
0 comments:
Post a Comment