MSANII anayeshikilia nafasi ya juu kwa sasa kwenye muziki wa kizazi kipya Tanzania Nasseb Abdul ‘Diamond’, inasemekana kuwa ameamua kutoa ya moyoni juu ya Wema Sepetu katika ngoma yake mpya ya ‘Nataka Kulewa’,
ambayo imezungumzia matukio yote yaliyomkuta alipokuwa na mwanadada
huyo na mengine ambayo yalikuwa yanazungumzwa na watu pindi wakiwa
wapenzi.
Chanzo kimoja cha karibu na msanii huyo kilizungumza na ...., kilidai kuwa mistari yote inayopatikana ndani ya ngoma hiyo ni matukio ambayo Diamond alikuwa ameyafanya kwa Wema na mengine ya kusikitisha ambayo awali yalikuwa yanazungumzwa na yeye alijua uzushi.
Chanzo hicho kilidai kuwa Diamond ameamua kutoa ngoma hiyo ili itoe ujumbe kuwa yote waliyokuwa wanafanya ni ujinga wake na anashukuru kwa kumfanywa kama zezeta katika mapenzi yao kwani alikuwa anaambiwa lakini hakusikia.
Baadhi ya maneno yanayopatikana ndani ya ngoma hiyo yanasema kuwa ‘mwanzo sakuamini nilijua vya kuzua, kumbe mjinga ni mimi ninayetunza wenzangu wanachukua, mapenzi mapenzi yalinifanya niliye vibaya kama mtoto, yaliyonikuta niache niseme yamenikaa moyoni.’
Mengine ni ‘nikamvisha na pete ya kumuoa kukata vilimilimi vya wazushi na wanafiki wanaomponda, kumbe mwenzangu na mimi ni bure tu najisumbua, sisi tupo kama 20 mabuzi, ving’asti na wengine wa anawahonga,’ ni baadhi ya maneno mazito yanayopatikana ndani ya ngoma hiyo
Kutokana na baadhi ya maneno hayo ukiyafuatilia mapenzi ya Diamond na Wema yalivyokuwa utajua ni maneno ambayo yamejaa ukweli juu ya mahusiano yao ambayo yaliteka watu wengi hasa pale alipomvisha pete Wema