Mbunge Mr II, Sugu anayetaka Rick Ross alipe kodi kwa pato lake la leo Fiesta |
Rick Ross atakuwa kulipa kodi |
MWANAMUZIKI
nguli wa Hip hop Tanzania na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Osmund Mbilinyi
amewapa mwongozo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu ziara ya mwanamuziki
nyota wa Hip hop Marekani, William Leonard Roberts II anayetambulika kama Rick
Ross au The Boss, kwamba anastahili kulipa kodi kutokana na pato atakalaolingiza
katika shoo yake ya leo.
Rick Ross atatumbuiza
usiku wa leo katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye viwanja vya Leaders
Club, Kinondoni, Dar es Salaam, ambalo linaandaliwa na Prime Time Promotions na
kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Mbunge Mbilinyi
ambaye anajulikana kwa majina ya kimuziki kama Mr II au Sugu, ameandika kwenye
ukurasa wake wa Facebook; “RICKY ROSS ANAKUJA, SAWA HAINA SHIDA…ILA TUNATAKA
KUJUA AMELIPWA KIASI GANI NA ATAKATWA KIASI GANI KIBAKI KWENYE KODI YA TAIFA
LETU KAMA AMBAVYO MIMI NIKIENDA KUFANYA SHOW/CONCERT MAREKANI NAKATWA KODI NA
SERIKALI YAO…”.
The Boss,
ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki watakaohudhuria tamasha la Serengeti Fiesta
2012 jioni ya leo kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.
Rapa huyo,
aliyefikia katika hoteli ya Hyatt, zamani Kilimanjaro Kempensky, Dar es Salaam,
ambaye alizaliwa JanuarI 28, mwaka 1976 huko Carol City, Florida, Marekani
alisema hayo baada ya kutua Dar es Salaam usiku wa jana.
“Rick Ross
ametua na ameahidi kufanya shoo kali sana,”alisema Allan Chonjo, Meneja wa Bia
ya Serengeti, wadhamini wakuu wa Fiesta.
Rapa huyo
mwenye miraba minne, ambaye ana bifu kali na Curtis Jackson ’50 Cent’ aliyewahi
kuzuru Tanzania pia, aliwasili Dar es Salaam usiku wa jana na anatarajiwa
kuwapagawisha wapenzi wa Serengeti Fiesta kwa nyimbo kali kutoka kwenye albamu
zake za Port of Miami aliyoitoa mwaka 2006, Trilla ya 2008, Deeper Than Rap ya
2009, Teflon Don ya 2010 na God Forgives, I Don't ya mwaka huu.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, wadhamini wakuu wa Serengeti Fiesta 2012, Ephraim
Mafuru Balozi alisema kwamba wanajisikia fahari kubwa kwa bia ya Serengeti kuwa
mdhamini mkuu wa tamasha hilo kwa muda wa miaka minne sasa.
“Bia ya
Serengeti inafahamika kwa umahiri wake katika ubora na ladha yake.
Imejinyakulia medali za dhahabu kutoka katika mashirika ya ushindanishaji bia
duniani DLG na Monde na pia ni fahari kwa kuwa bia ya kwanza Tanzania kuwa na
kimea cha asilimia 100. Bia hii imejiwekea historia ya kuwa bia inayokua kwa haraka
katika ujazo na thamani yake,”alisema Mafuru.
Mkurugenzi huyo
aliwaomba wakazi wa Dar es Salaam kujitokeze kwa wingi jioni ya leo katika
viwanja vya Leaders Club wakaburudike na muziki wa vijana wa Tanzania na pia
kumshuhudia mwanamuziki Rick Ross kutoka Marekani. “Pia tunawahakikishia kwamba
watapata bia ya Serengeti yenye muonekano mpya, na ladha yake ni ile ile yenye
ubora thabiti. Kwa hiyo watapata bia yenye muonekano tofauti, burudani ile ile,”alisema.
Mafuru aliongeza; “Tunazo Bia za aina
nyingi kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti pia zitakuwepo kama vile;
Tusker Lager, Pilsner Lager, Tusker Malt Lager, Uhuru Peak Lager, Smirnoff Ice
Black na Red, na kwa wanaopendelea vinywaji vikali watapata Johnnie Walker
Whisky, Smirnoff Vodka, VAT 69, Captain Morgan, Baileys na Gilbeys Gin. Pia kutakuwa na vinywaji visivyo na kilevi
cha Malta Guinness na Alvaro. Tumejiandaa
vya kutosha kuwapatia vinywaji hivyo kwa bei ya shilingi 1,800 tu,”alisema.
0 comments:
Post a Comment