Mtu mzima Rick Ross “The Boss”
kutoka nchini Marekani akiwa jukwaani kwenye Tamasha la
Serengeti Fiesta 2012 lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni
jijini Dar salaam ,akikamua ile mbaya na mashabiki wamepagawa
vyakutosha kwa kila anachowaelekeza kufuata wanafuata jamaa amefunika
mbaya, hiii ni mara yake ya kwanza kufanya onesho nchini Tanzania
Rachel Mwanamuziki wa
Bongofleva kutoka kundi la THT akicheza na mmoja wa wacheza shoo wake
katika Tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku kwenye
viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambapo pamoja na wasanii
mbalimbali wakali wa nyumbani, mwanamuziki maarufu wa Hiphop kutoka
nchini Marekani Rick Ross “The Boss” atahitimisha tamasha hilo kwa shoo
kali usiku wa kuamkia leo .
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani
Rick Ross akiimba jukwaani usiku wa kuamkia leo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji
la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club,wakati wa
tamasha la Serengeti Fiesta likirindima.
Mkali mwingine wa miduara AT na madansa wake wakilishambulia jukwaa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,akiimba jukwaani na shabiki wake.
Mashabiki wakitaka kuangusha uzio uliowekwa kwa ajili ya usalama.
Baadhi ya Askari wakijaribu kuweka
usalama wa kutosha kwa Mwanamuziki Rick Ross imara baada ya kuwasili
kwenye viwanja vya Lidaz Club,kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la
Serengeti Fiesta 201.
Viwanja vya Lidaz palikuwa hapatoshi hata kidogo.
Mwanamuziki kutoka nchini
Marekani,Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona Watanzania wakiwa
wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye akikamua stejini.
Watu kibao wakiwa ndani ya viwanja vya lidaz club usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa miondoko ya rusha rohoo
a.k.a Miduara,Shilole akijiachia jukwaani vilivyo na madansa wake usiku wa kuamkia leo mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye viwanja vya Lidaz Club,katika
kuhitimisha kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
0 comments:
Post a Comment