Bunjak kulia akiwa na Kali Ongala na Daktari wa timu katika mechi ya juzi dhidi ya Simba |
Na Bin
Zubeiry Blog
KOCHA
Mserbia wa Azam FC, Boris Bunjak amefukuzwa rasmi leo na sasa aliyekuwa kocha wa
timu hiyo, Muingereza Stewart Hall anarudishwa
kazini.
Habari
kutoka ndani ya Azam FC zimesema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni
kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya
nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Tayari
Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka Alhamisi, siku ambayo Stewart
atawasili kuanza tena kazi Azam FC.
Bunjak
anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote
dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare
tatu.
Bunjak
mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka
huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla
ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor
Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi
Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na
Al-Nasr.
Awali,
Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika
klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac),
FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK
Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
Stewart
alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo,
kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya
Yanga.
Mserbia huyo
anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza
Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na
Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini
Stewart angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha
kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu
Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame miezi miwili
iliyopita, mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe
tena.
Stewart ana
sifa ya kutokuwa mbinafsi na mwenye kuwaamini watu wa chini yake, kwa mfano
namna ambavyo alikuwa akimpromoti Kali Ongala. Alimkuta Kali kama mchezaji,
lakini kwa sababu ya umri kumtupa mkono, akashauriana naye awe Kocha Msaidizi na
mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, akakubali.
Chini ya
Stewart, Kali alikuwa akiachiwa timu aiongoze ili kumjengea kujiamini zaidi na
mwezi uliopita aliachiwa timu kwenye Kombe la Urafiki, akaifikisha fainali,
ambako ilifungwa na Simba kwa penalti kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
WASIFU WA
BORIS BUNJAK:
JINA KAMILI:
Boris Bunjak
KUZALIWA:
Novemba 17, 1954 (Miaka 57)
KLABU
ALIZOCHEZEA:
1967- 1975:
FK Sloga (Kraljevo)
1975- 1978
FK Vozdovac (Beograd)
1978- 1979
FK Radnicki (Kragujevac)
1979- 1980
FK Olimpia (Ljubljana)
1980- 1981
FK Sumadija (Arandjelovac)
1981- 1985
FK Sloga (Kraljevo)
1985- 1986
FK Borac (Cacak)
1986- 1990
FK Sloga (Kraljevo)
KLABU
ALIZOFUNDISHA:
1990-1993:
FK Sloga (Kraljevo)
1995-1996:
FK Javor (Ivanjica)
1996-1997:
Crvena Zvezda (Gnjilane)
1999:
FK Radnicki (Nis)
2000:
FC Uralan Elista (Urusi)
2000-2002:
FK Mladi (Radnik)
2002-2004:
FK Crvena Zvezda (Beograd)
2004:
Al-Shaab (UAE)
2005:
FK Hajduk (Kula)
2006-2007:
Al-Nasr (Oman)
2009:
Al Oruba Sur (Oman)
2011:
FC Damac (Saudi Arabia)
2011:
AL NASER (Oman)
REKODI YA
BORIS BUNJAK AZAM
Azam 2-1
Polisi (BancABC)
Azam 1-2
Simba B (BancABC)
Azam 8-0
Trans Camp (Kirafiki)
Azam 1-0
Prisons (Kirafiki)
Azam 2-0
Coastal Union (Kirafiki)
Azam 2-3
Simba SC (Ngao ya Jamii)
Azam 1-0
Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Azam 2-2
Toto African (Ligi Kuu)
Azam 3-0 JKT
Ruvu (Ligi Kuu)
Azam 1-0
Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
Azam 1-0
African Lyon (Ligi Kuu)
Azam 2-3
Simba SC (Kirafiki)
Azam 1-0
Polisi (Ligi Kuu)
Azam
0-0 Prisons (Ligi
Kuu)
Azam 1-1
Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
Azam 1-3
Simba
(Ligi Kuu)
0 comments:
Post a Comment