UNAJUA KWAMBA BONDIA ORLANDO CRUZ NI SHOGA
Orlando Cruz kulia akizichapa na Cornelius Lock kuwania ubingwa wa NABO Latino uzani wa Featherweight.
SAN JUAN, Puerto Rico
BONDIA wa uzani wa ‘featherweight’ raia wa Puerto
Rico, Orlando Cruz amekuwa nyota wa kwanza wa masumbwi kuanika
hadharani ukweli kwamba yeye ni shoga.
Cruz, 31, alikuwa sehemu mabondia wa nchi hiyo walioshiriki
katika michezo ya Olimpiki 2000 na kupambana mapambano kadhaa ya kuwania
ubingwa dunia wa WBO.
"Nimekuwa mpambanaji ulingoni kwa zaidi ya miaka 24 sasa
nab ado ningali nataka kuendelea katika hilo,
lakini ni bora nikawa wazi kuhusu masuala yangu binafsi," alisema Cruz, ambaye
ameshinda mapambano 18 kati ya mara 22 alizopanda ulingoni.
"Mimi daima najisikia na nitaendelea kujisikia fahari
kuwa raia wa Puerto Rico. Na daima mimi
nimekuwa na nitaendelea kujivunia kuwa mwanaume shoga."
Kukiri ushoga kwa Cruz, kumekuja wiki mbili tu kabla ya
mkali huyo kupanda ulingoni kumvaa Jorge Pazos kuwania ubingwa wa WBO Latino uzani
wa ‘featherweight’ huko Florida,
pambano linaloweza kumpa tiketi ya kuwania ubingwa wa dunia.
Cruz aliongeza katika mahojiano yake kuwa: "Nataka
kujaribu kuwa mtu wa kuigwa na vizazi vyote wakiwamo watoto katika suala zima
la mchezo wa masumbwi ya kulipwa na si vinginevyo."
Bingwa mara mbili wa zamani wa dunia Emile Griffith, aliwahi
kukiri kuwa yeye ni shoga katika mahojiano aliyoyafanya na jarida la Sports
Illustrated, lakini alifanya hivyo wakati akiwa ameshastaafu mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment