MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa
kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi
ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.
Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo
ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na
wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma
mwakilishi wake.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika
Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika
mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti
2, mwaka huu.
Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa
Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu
uongozi huo.
Kwa
mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa
mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi
huo kupitia blogu yake.
Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/07/angalia-picha-jide-na-mumewe-gadner.html#ixzz2aYMg3cyr
0 comments:
Post a Comment