Ushindani wa biashara ya smart phone unazidi kukuwa na kufanya kila
kukicha makampuni pinzani kama Samsung na Apple kuja na matoleo mapya ya
bidhaa zao zinazoleta ushindani mkubwa wa soko. Kampuni ya Samsung
imepeleka sokoni toleo jipya la Galaxy S4 Active isiyongia maji wala vumbi ‘waterproof and dustproof version’.
Kampuni ya Samsung yenye makao yake makuu Korea kusini imesema
imetengeneza toleo hili la Galaxy S4 Active isiyopitisha maji wala
vumbi, ikiwalenga wazazi kwa kuwasaidia kuepusha ajali na uharibifu
unaoweza kusababishwa na watoto.
“We know a lot of parents use their phones to show children
content. We ended up going to a lot of family homes where we were shown a
graveyard of smashed phones”. Alisema Luke Mansfield mkuu wa ‘ Samsung’s Europe innovation team’ alipozungumza na The Times.
Simu hiyo inauwezo wa kukaa ndani ya maji kwa dakika 30 na kupiga picha majini kwa kutumia ‘waterproof camera’.
Simu ya Galaxy S4 Active ambayo ilitambulishwa (May) imeingia sokoni
mwezi huu (July) na inagharimu £480 sawa na karibia million 1 na laki
2.
0 comments:
Post a Comment