Sura ya
mauzo kunako gemu la filamu za Kibongo, Wastara Juma amefunguka kuwa
wanaume wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’
akiwa mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi.
Akizungumza
kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi
Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye
wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo
ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.
Bishosti huyo alisema kuwa tofauti na wanaume hao ambao walikuwa
wakimpa sapoti kipindi hicho, bado wapo wengine kibao kutoka nje na
ndani ya nchi ambao wanatuma maombi kwake lakini anawaona wote ni
matapeli na wanamtamani tu hivyo hayupo tayari kuingia kwenye uhusiano
wa aina hiyo.
“Kweli
ninaumia sana kwa sababu ninakaa na kujiuliza hawa wanaume walikuwa
wanasubiri mume wangu afariki dunia ndiyo wanitongoze?
“Kusema
kweli inanishangaza, hata watu ambao sikuwadhania kabisa eti nao
wananitaka, watu wajue kwa sasa sipo tayari kuwa na mwanaume.
“Sitaki
kukurupuka kwa sababu naweza nikaingia kwenye shimo la taka kwani jamii
itanikimbia kutokana na kunuka, natamani kumpata mwanaume anayefanana
na mume wangu kitabia.
“Uvumilivu
wangu na uzuri ulitokana na kutunzwa siyo aje mtu anayetaka nikavumilie
shida, hilo sitaki litokee, namuomba Mungu sana,” alisema Wastara.
Kwa
upande mwingine, staa huyo alisema kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu
kutokana na upweke na kama angekuwa hana watoto, angeomba afe akapumzike
kwani faraja yake kubwa ilikuwa ni Sajuki lakini baada ya kutwaliwa na
Mungu watoto ndiyo wamechukua nafasi hiyo.
Wastara
aliwaomba watu wote wakimuona wasioneshe huzuni kwani ndiyo anaumia
zaidi badala yake wawe na furaha kwani tangu aliporudi kutoka Uarabuni
mawazo ya marehemu Sajuki yamekuwa yakimrudia mara kwa mara kutokana na
kukutana na stori na maswali yaleyale.
Baadaye,
tuliwasiliana na Wastara na kumuuliza kama miongoni mwa wanaomtaka
kimapenzi wapo wafanyakazi wa Global Publishers kwani ni miongoni mwa
waliomsaidia ambapo alijibu kuwa hawahusiki.
“Jamani Global hamhusiki nilimaanisha mtu mmojammoja na wenyewe pia siyo wote ni baadhi yao,” alisema.
Wastara alifiwa na mumewe Sajuki Januari 2, mwaka huu baada ya kumuuguza kwa muda mrefu.
kwa hisani ya: audifacejackson.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment