Maelfu ya wananchi walikusanyika katika miji zaidi ya 100 marekani siku ya Jumamosi
(July 20) kupinga "Stand Your Ground Law" katika kumsapoti Trayvon Martin, kijana mweusi mwenye miaka 17, ambae alipigwa risasi na kuuwawa na George Zimmerman 2012.
hiphop most famous couples, Jay Z na Beyonce pia waliungana na wananchi hao.
Jay
na Beyonce walihudhuria uhasamishaji huo wakiwa Manhattan, New York
wakiongozana na Al Sharpton (Baptist Minister, Civil Rights/social
justice activist, Radio and Tv talk show host) na mama mzazi wa kijana
alieuwawa Sybrina Fulton.
"Jay-Z na
Beyonce wamesema, hawakutaka kuongea, hawakuja kwa ajili ya kuonekana
kwenye picha" amesema Al Sharpton, "Jay Z ameniambia mimi ni baba.
Beyonce ni mama. Wote tunahisi uchungu na wasiwasi- sheria lazima
zimlinde kila mtu, au isimlide yoyote, hatujaja kwa ajili ya chuki,
tumekuja kwa ajili ya mapenzi na watoto"
Zimmerman
alikutwa hana hatia ya mauaji ya shahada ya pili au bila kukusudia baada
ya kesi hiyo kuendeshwa na kuonyeshwa live kupitia television ya taifa.
baada
ya uamuzi kutangazwa kuwa Zimmerman hana hatia, emcees kama vile
Technique Immortal, Brother Ali, Young Jeezy, na SpaceGhostPurrp,
miongoni mwa wengine wengi, haraka walipingana na na habari.
0 comments:
Post a Comment