DENTI
mmoja wa Shule ya King'ong'o jana aliadabishwa na Mwenyekiti wa Serikali
za Mitaa King'ong'o aliyejulikana kwa jina la Mapesi baada ya kumkuta
barabarani akiwa amesimamishwa na wavulana badala ya kwenda nyumbani.
Mwanafunzi huyo alipomuona mwenyekiti alijaribu kukwepa huku wavulana aliokuwa nao wakikimbia kwa kuhofia tabia yao lakini alishindwa kwani mwenyekiti alifanikiwa kumkamata mikononi na kumtia 'displine'.
Mwanafunzi alipobanwa alidai kuwa alikuwa amemfuata mvulana mmoja ambaye zamani alikuwa mpenzi wake na alifika eneo hilo baada ya kumuita.
Hata hivyo mwisho aliomba msamaha na kumpigia magoti mwenyekiti huyo ili aondoke na kuelekea nyumbani kwao.
0 comments:
Post a Comment