Muigizaji Wentworth Miller maarufu zaidi kama Michael Scolfield kwenye tamthilia ya Prison Break, ametangaza kuwa shoga.
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa kwenye mtandao wa People.com,
Wentworth ameweka wazi taarifa hiyo kwenye barua aliyoandika kukataa
mwaliko kuhudhuria tamasha la filamu la la kimataifa la St. Petersburg
nchini Urusi.
Barua hiyo ilichapishwa kwenye mtandao wa ‘Gay and Lesbian Alliance Against Defamation’.
“Asante kwa mwaliko wenu. Kama mtu niliyefurahia kuitembelea Urusi
miaka ya nyuma na ambaye nina asili kiasi ya Urusi, ingenipa furaha
kusema ndio,” aliandika. “Hata hivyo, nikiwa kama shoga ni lazima
niukatae.”
Aliongeza, “Ninakerwa kwa kiasi kikubwa na jinsi mashoga
wanavyotendewa na serikali ya Urusi. “Hali ilivyo haikubaliki kwa namna
yoyote na siwezi kushiriki kwa amani kwenye tukio linaloandaliwa na nchi
ambako watu kama mimi wananyimwa haki yao ya msingi ya kuishi na
kupenda kwa uwazi. Pengine, pindi mambo yakibadilika, ntakuwa huru
kuchukua uamuzi tofauti.”
Barua hiyo imetokana na sheria dhidi ya ushoga iliyosainiwa na rais
Vladimir Putin wa Urusi. Urusi ilipitisha sheria hiyo mwezi uliopita
inayozuia mijadala ya wazi kuhusu haki na mahusiano ya jinsia moja
popote pale ambapo watoto wanaweza kusikia.
Mwezi June, nchi hiyo ilianzisha sheria inayokataza kuasiliwa
(adoption) kwa watoto wa Urusi na wapenzi wa jinsia moja wanaoishi
katika nchi inayokubali sera za mahusiano hayo, lesbian, gay, bisexual,
and transgender, LGBT.
Wentworth alijipatia umaarufu kwenye tamthilia ya Prison Break ya
mwaka 2005 hadi 2009. Pia ameandika na kushiriki kutayarisha filamu ya
mwaka huu iitwayo Stoker, aliyoigiza Nicole Kidman.
0 comments:
Post a Comment