Wapita
Njia walipata hali ya kutishwa wakati mtu huyo, ambaye alisemekana
kuwa maiti, ghafla aliamka na kumpora mmoja wa waombolezaji chupa ya
maji na kuanza kunywa.
Raia
huyo wa China alidanganya kifo chake mwenyewe ili kuishitaki serikali
baada ya mabishano na wafanyakazi wa serikali ambao inasemekana
walimpiga, basi akafanya uongo huo ili apate fidia ya Kifo hicho.
Lakini mpango wake uliingia dosari kutokana na Hali ya Joto Kali katika Mkoa wa Hubei, Huko China ya kati.
Tukio
hilo lilitokea majira ya saa Kumi Alasiri wakati zaidi ya watu 10
wakiwa wamembeba maiti huyo huku akiwa kufunikwa na karatasi nyeupe
karibu na kituo cha Jianghan Road Subway katika mji mkuu wa mkoa wa
Wuhan.
Zaidi ya watu 300 waliokusanyika katika eneo la tukio, na maafisa wa polisi 80 walipelekwa eneo la tukio ili kudumisha amani.
Baada
ya masaa mawili ya maandamano, "Maiti" Mtu huyo ghafla alisimama,
akaipora chupa ya maji ya kunywa na kusema: "Ni Joto sana, siwezi
kuvumilia ".
Maiti huyo aitwaye Han, pamoja na wenzake wawili wengine, wamekamatwa kwa kitendo chao hicho.
chanzo:audiface jackson
0 comments:
Post a Comment