Na Andrea ngobole,Arusha
NAIBU katibu mkuu wa jumuiya ya Africa Mashariki (EAC),Jesca
Eriyo ametoa wito kwa vijana wa jumuiya hiyo kuweza kujituma na kujikita katika
kilimo cha kisasa ili kiweze kuwakomboa na wimbi la umaskini linalowakabili
vijana hapa Nchini
Eriyo alitoa rai hiyo mwishoni mwa juma wakati akizundua kongamano
la vijana wa jumuiya hiyo,katika ukumbi wa Light in Afrika uliopo wilayani Hai
Mkoani Kilimanjaro,lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Vission
for Youth lenye makao yake makuu Mkoani
Arusha na kukutanisha vijana 120 kutoka nchi wanachama.
Aidha alibainisha
kuwa ili kijana aweze kujikwamua kimaisha inamlazimu kujikita katika sekta ya
kilimo cha kisasa ambapo jumuiya imeamua kuwaunga mkono vijana kwa kutoa fursa
ya kuwatafutia masoko katika nchi wanachama ili waweze kuvuka mipaka na
kujitangaza kupitia biashara wanazozifanya.
Alisema kuwa vijana
wanatakiwa kutambua kuwa kilimo ndiyo sekta pekee ambayo inaleta ajira ya moja
kwa moja kwa kijana na familia kwa ujumla,kwani kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa,kwani hivi sasa
kilimo huliingizia pato Taifa kwa asilimia kubwa huku akibainisha kuwa kilimo
hapa Nchini kinategemewa na wananchi kwa asilimia 75.
“mkitumia kilimo cha kisasa mtapata faida kwani kwa kutambua
mchango wa kilimo Jumuiya ya Afrika mashariki imeweka mipango mathubuti ya
kuwatafutia masoko katika nchi wanachama kwa kuondoa vikwazo vya ushuru
barabarani na katika mipaka ya kutokea kutoka nchi moja kwenda nchi
nyingine”alisema Eriyo
Aidha alisema ili vijana waeze kufankiwa wanatakiwa kuepuka kutumia madawa ya kulevya (unga) ambayo
yamekuwa yakiwadhoofisha afya na kukosa nguvu ya kutimiza ndoto zao ,kwani
kijana akitumia madawa hayo anaweza kuathirika na magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Ukimwi na
magonjwa ya mengine.
Alisisitiza pia kuwa vijana waliopo vijijini wanaweza
kunufaika na soko la pamoja katika jumuiya hiyo,kwa kuuza bidhaa zao nje ya
nchi,kwani miundo mbinu imeboreshwa katika nchi wanachama wa jumuiya ya
hiyo,kuanzia mawasiliano ya simu,barabara, na kutolazimika kuwa na kibali cha
kazi katika nchi wanachama.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi huo,Afisa
miradi wa shirika la Vission for Youth Vedastus Sibula,alisema changamoto
inayowakabili vijana kwa hivi sasa ni kuogopa kutumia fursa zinazopatikana
katika jumuiya hiyo,hivyo kwa kutambua hilo wameamua kuandaa kongamono la siku
tatu,likishirikisha vijana kutoka Amerika,Uingereza,Tanzania, Uganda na Kenya likiwa
na lengo la kuwapa fursa za zinazoweza kuwainua katika sekta ya kilimo cha
kisasa.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment