Mgambo
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na viongozi mbali mbali
wakielekea kuvunja nyumba zilizojengwa makaburi ya Mtwivila leo
Mgambo
wa Manispaa ya Iringa na mwanasheria katikati Bw Innocent Kihaga
wakielekea kuvunja nyumba zilizojengwa makaburini Mtwivila
Mgambo wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakivunja nyumba iliyojengwa katikati ya makaburi ya Mtwivila
Hii
ndio nyumba ambayo ipo jirani na kaburi la marehemu Idd Chonanga
aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli kaburi lenye mashada kushoto ,na
hapo waliposimama mgambo ndipo alipokaa waziri mkuu Mizengo Pinda
wakati wa mazishi na viongozi mbali mbali wa mkoa wa Iringa
Uvunjaji wa nyumba wa nyumba ukiendelea huku mmiliki wake amepewa siku 30 kuanzia leo kuivunja
Wananchi ambao wamezika ndugu zao katika makaburi hayo wakishuhudia zoezi hilo
HATIMAYE
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeivunja nyumba iliyokuwa
ikijengwa katikati ya makaburi ya Mtwivila ambayo iliripotiwa na
mtandao huu na vyombo mbali mbali vya habari likiwemo gazeti la
Jamboleo , radio Ebony Fm na radio Cloud FM pamoja na nyumba
nyingine mbili ambazo pia zilikuwa zikianzwa kujengwa eneo hilo .
Pamoja
na kuendesha zoezi la kuzivunjwa nyumba hizo ambazo zilikuwa
katika hatua ya mwanzo kabisa pia Halmashauri hiyo imetoa muda wa
siku 30 kuanzia leo kwa mmiliki wa nyumba nyingine iliyokutwa
imekamilika ambayo pia imejengwa karibu na makaburi ya Mtwivila eneo
ambalo waziri Mkuu Mizengo Pinda alikaa wakati wa mazishi ya
aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli marehemu Iddi Chonanga
Hatua
ya kuvunjwa kwa makaburi hayo imekuja ikiwa ni siku mbili
zimepita baada ya mtandao huu wa matukio daima kuibua suala hilo
kuibua ujenzi huo holela na ni siku moja baada ya mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya Manispaa Bi Terresia Mahongo kutoa agizo
kwa maofisa mipango miji , afisa ardhi na mwanasheria wa Manispaa
ya Iringa kufika eneo hilo ili kuchukua hatua sitahiki.
Zoezi
la kuvunja nyumba hizo leo majira ya saa 3 asubuhi limeongozwa na
maofisa mbali mbali wa Manispaa ya Iringa akiwemo mwanasheria wa
Halmashauri hiyo Bw Innocent Kihaga pamoja na mgambo zaidi ya watano
wa Halmashauri hiyo.
Kuvunjwa
kwa nyumba hizo kumeshuhudiwa na umati mkubwa wa wananchi wa
maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa ambao walifika kushuhudia
utekelezaji wa agizo la mkurugenzi baada ya baadhi yao kudai
wamiliki wa nyumba hizo wamejenga katika makaburi ya ndugu zao
hivyo walikuwa wakishindwa kuchukua hatua kutokana na kutojua
wahusika wa ujenzi huo wa nyumba makaburini.
na fransicgodwinblogspot
0 comments:
Post a Comment