Mamlaka
ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) imeanza kuchukua hatua dhidi ya
wafanyakazi wanaotuhumiwa kuwasaidia Agnes ‘Masogange’ Gerald na mdogo
wake Melisa Edward kupitisha dawa za kulevya katika uwanja wa JNIA
(July 5).
Hatua hiyo inafuatia agizo la Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison
Mwakyembe aliyeitaka Mamlaka hiyo kuwachukulia hatua za kisheria wale
wote waliohusika kula njama ya upitishwaji wa dawa hizo aina ya
Crystal Methamphetamine, zilizoenda kukamatiwa katika uwanja wa ndege
wa OR-Tambo, Afrika Kusini.
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA),
Moses Malaki, amesema wafanyakazi wanaotuhumiwa kula njama hiyo
watasimamishwa kazi wakati wowote kuanzia leo kabla ya kupewa nafasi ya
kujitetea kwenye tume itakayoundwa kuwachunguza.
Malaki ambaye awali alionyesha kushangazwa na kiasi kikubwa cha dawa
hizo kupita, alisema utaratibu unakamilika wa kuundwa tume na
kuwasimamisha kazi wahusika.
“Baada ya tume kukamilika na kupewa hadidu rejea, tutawaita mmoja
mmoja kwenye kujieleza, hapo tutajua kama wahusika watakuwa na hatia
au la,” alisema.
Alisema baada ya kumaliza kazi, tume itatoa maelekezo kwa Serikali kinachotakiwa kufanyika.
Ijumaa iliyopita (August 16) Dk. Mwakyembe alizungumza na waandishi wa habari kuelezea jinsi dawa hizo zilivyopitishwa uwanjani hapo,
na kuiagiza TAA kuwafukuza kazi mara moja wafanyakazi wake wanne
waliohusika katika mpango huo, kisha kuwakamata na kuwaunganisha katika
mashitaka yanayowakabili.
SOURCE: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment