Arusha:
TAMASHA la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa
kufanyika Septemba 8 katika viwanja vya General tyre Arusha na
kushirikisha waandishi kutoka jijini Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro
na mkoa wa Manyara.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za
michezo mkoa wa Arusha(TASWA) Mussa Juma, alisema zaidi
ya waandishi wa habari na wadau wa habari 500 wanatarajiwa kushiriki
katika Tamasha hilo.
Juma
alisema kwa upande wa michezo timu ambazo zitashiriki ni TASWA FC
kutoka jijini Dar es Salaam, TASWA Arusha, Radio Sunrise, Radio 5, Radio
Triple A, Arusha One Radio na Chuo cha Uandishi wa habari Arusha ambao
ndio mabingwa watetezi.
Alisema
pia kutakuwa na timu ambazo zimealikwa ambazo ni timu ya TBL Arusha
ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, timu ya Wazee
Klabu,Kitambi Noma, Timu ya Pepsi na timu ya NSSF Arusha.
Juma
alisema katika tamasha hilo, ambalo huandaliwa na TASWA na kampuni ya
Ms Unique, kutakuwa na michezo ya soka, kuvuta kamba, kukimbiza kuku,
mpira wa mikono na mbio za magunia.
Alisema
Septemba 7 bonanza hilo, litatanguliwa na semina ya siku moja kwa
waandishi wa habari mkoa wa Arusha kuhusiana na sheria za michezo,
masuala ya afya na jinsi ya kutumia michezo katika kutangaza
utalii.
Hata hivyo, Juma alisema bado wadhamini wanaombwa kujitokeza kudhamini tamasha hilo.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment