Wiki
iliyopita Diamond Platnumz alisababisha timbwili zito mjini Mombasa
baada ya kuchelewa kupanda kwenye steji ya show yake na kusababisha
mashabiki kuanza kurusha chupa.
Kupitia kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen, Diamond amefunguka kuhusu sababu ya yeye kuchelewa kupanda stejini.
“Nililipwa pesa nusu, nikawa natakiwa nikifika Nairobi nimaliziwe
pesa yangu yote iliyobaki lakini baada ya kufika Nairobi nikafanya show
nikapewa pesa tena nusu iliyobaki sikupewa,” amesema Diamond.
“So kufika Mombasa nikasema siwezi kupanda kwenye stage mpaka
nimaliziwe pesa yangu sio, kwasababu ilikuwa imebaki kama dola elfu sita
na kitu, saba kasoro hivi. Nikasema mpaka nimaliziwe pesa yangu ndio
nipande kwenye stage. Sababu kulikuwa na uongo uongo kidogo, ‘ukishuka
utapewa’ unajua sisi wasanii tulishadhulumiwaga sana, mtu huwezi
kumwamini kwamba upande stejini halafu ushuke, lazima upewe chako.
Nikasema ‘mimi nataka mnilipe hela yangu ndio nipande kwenye stage’.
Halafu wakati huo show imejaa, sijawahi kuona show iliyojaa hivyo. So
baada ya kukamilishiwa pesa yangu ndio nikatoka nikaenda stejini saa
tisa hiyo na kitu. Before kabla sijafika watu walikuwa wameshaanza
kufanya vurugu, watu walipiga machupa nasikia, vurugu kinomanoma. Lakini
namshukuru mwenyezi Mungu nilipofika mimi zile jaziba zote zikapungua
watu walikuwa na mizuka.”
0 comments:
Post a Comment