Blogger Widgets

Thursday, November 22, 2012

Cheki Dude lililodondoka usiku wa manane Kijiji cha Ruganzo wilayani Ngara mkoani Kagera na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi.

 

Kitu kinachosadikiwa ni bomu

     Wataalamu wa mabomu kutoka Jehsi la wananchi wa Tanzania JWTZ kambi ya Biharamulo wameanza kazi ya kukagua kitu ambacho kimeanguka kwenye eneo la Ruganzo wilayani Ngara mkoani  Kagera.

Kituo hicho ambacho baadhi ya watu wanasadiki kuwa ni bomu kina ukubwa wa sentimeta 50 na umbo kama la yai huku kikiwa na nyuzinyuizi kimeanguka jana usiku katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu amesema wataalamu hao wa mbomu ndio watabaini kitu hicho na kuweza kukitolea maelezo pmoja na hatua za kuchukua.
 
Wapo waliodhani kuwa kitu hicho
ni Kombora la masafa marefu
 lililorushwa kutoka nje ya Nchi

 Ni kitu kisichofahamika ni nini, Wapo waliodhani kuwa kitu hicho ni Kombora la masafa marefu lililorushwa kutoka nje ya Nchi,wapo waliodhani kuwa ni Kimondo,wapo wanaodhani kuwa ni Satelite!..LAKINI  Majibu yatatolewa katika Ripoti itakayotolewa na timu/kikosi cha wanajeshi naohusika na masuala ya Mlipuko. tayari kikosi kutoka Biharamulo kimeagizwa KUCHUNGUZA.

Eneo la Ruganzo

   
Kitu hicho kilichondoka kutoka angani hadi ardhini Usiku wa Jumatano November 21 kuamkia Alhamisi November 22, 2012 saa nane Usiku na  kuleta kishindo kikubwa kilichopelekea hali inayofanana na tetemeko la ardhi,wakazi wengi wa eneo la Ruganzo kata ya Kibimba wilayani  Ngara mkoani Kagera  wamekumbwa na hofu kutokana na kitu hicho.
Aidha  kwa mujibu wa mkuu wa Ngara Bw.Kanyasu AMEPIGIWA SIMU NA MAAFISA WA BURUNDI WAKIMUULIZA JUU YA MIUNGURUMO ILIYOSIKIKA UPANDE WA TANZANIA.

JWTZ WAMESHAFIKA ENEO LA TUKIO NA WANAENDELEA NA UCHUNGUZI ZAIDI. BADO HALIJARIPUKA. HUENDA WAKALITEGUA.
Chanzo:Radio Kwizera FM

0 comments:

Post a Comment