Kituo
cha Sheria na Utetezi wa Haki za Binadamu (LHRC) na Chama
Cha Wanasheria Tanzanyika vimefungua kesi ya Kikatiba katika Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, vikiomba mahakama hiyo itoe tafsiri za
kisheria katika baadhi ya Ibara.
Kesi hiyo ya Kikatiba ambayo imepewa
namba 24 ya mwaka huu, na ambayo bado haijapangiwa jaji, wadaiwa ni
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Taasisi hizo ambazo zinatetewa na mawakili wa kujitegemea Harold
Sungusia, Francis Stolla na wengine 17, kwa mujibu wa hati yao ya madai,
walalamikaji hao wamewasilisha jumla ya maombi mawili ambayo wanaomba
mahakama itoe tafsiri ya kisheria katika Ibara hizo kwa kuwa
wamewasilisha kesi hiyo ya Kikatiba chini ya sehemu ya Tatu ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo
inaainisha Haki na Wajibu Muhimu.
- Wakili Sungusia alilitaja ombi la kwanza kuwa, wanaiomba mahakama hiyo itamke kuwa ibara ya 100(1) ya Katiba ya nchi inayotoa uhuru wa majadiliano kwa wabunge wawapo ndani ya bunge ambayo inasomeka hivi: “kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katikaMahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.”
Wakili Sungusia anadai kuwa Ibara
hiyo ina ubaguzi ndani yake kwani inayoa uhuru kwa mbunge kujadili ndani
ya bunge na wakati anajadili jambo hata kama amevunja haki za mtu
mwingine hataweza kushitakiwa wala kuhojiwa jambo ambalo anadai
linakinzana na Ibara ya 13(2) ya Katiba ambapo Ibara hii inasomeka hivi;
“ Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika
Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa
dhahiri au kwa taathira yake’.
‘...sisi tunaomba mahakama itamke wazi kuwa Ibara ya 100(1) inakwenda
kinyume na matakwa ya Ibara 13(2). Zinakinzana, kwa kuwa ibara ya
100(1) ya Katiba inatoa haki tu kwa upande wa mmoja wa wabunge uhuru
wao kutohojiwa na inawanyima haki ya kuwahoji au kuwashitakiwa wabunge
wanaotoa kauli zao bungeni hata kama kauli hizo za wabunge zimevunja
haki za wananchi,”alidai wakili Sungusia.
- Wakili Sungusia alilitaja dai la pili kuwa ni kuiomba mahakama hiyo itamke kuwa kauli ya Waziri Mku, Pinda ambayo ililitaka Jeshi la Polisi kuwapiga wale wote wanaokiuka amri za jeshi hilo, kama kauli hiyo nayo inalindwa na kinga iliyowekwa katika Ibara ya Ibara ya 100(2) ya Katiba ya nchi ambayo inasomeka hivi: ‘Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.’
Katiba mkutano wa bunge uliomalizika hivi karibuni , Waziri Mkuu
Pinda akiwa ndani ya bunge aliliagiza jeshi la polisi kuwapiga wale wote
wanaokaidi amri za jeshi hilo, kwasababu serikali imeshachoshwa na
vitendo vya baadhi ya wananchi wanaokaidi kwa makusudi amri za jeshi la
polisi , kauli iliyoleta mhemko kwa jamii huku wengine wakiipinga
utekelezaji wa agizo hilo na wengine wakiunga mkono, hali iliyosababisha
LHRC hivi karibuni ilizungumza na waandishi wa habari wakimtaka Pinda
afute kauli yake hiyo ama sivyo watamfikisha mahakamani.
chanzo: http://audifacejackson.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment